Kaimu Meneja wa Wakala wa vipimo Tanzania WMA akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wazalishaji wa bidhaa na wafanyabiashara namna ya ufungashaji wa bidhaa na matumizi sahihi ya vipimo katika bidhaa.
Katibu Tawala msaidizi Mkoa wa Dodoma sekta ya uchumi Bi Aziza Mumba akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wazalishaji wa bidhaa na wafanyabiashara namna ya ufungashaji wa bidhaa na matumizi sahihi ya vipimo katika bidhaa.
Kaimu Meneja wa Wakala wa vipimo Tanzania Mkoa wa Dodoma Karim Zuberi akitoa maada wakati wa wa semina ya kuwajengea uwezo wazalishaji wa bidhaa na wafanyabiashara namna ya ufungashaji wa bidhaa na matumizi sahihi ya vipimo katika bidhaa.
Mmoja wa wanufaika wa semina hiyo ambeye ni mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wapambanaji Dodoma Bi. Marry Barnabas akizungumza mara baada ya semina kuwajengea uwezo wazalishaji wa bidhaa na wafanyabiashara namna ya ufungashaji wa bidhaa na matumizi sahihi ya vipimo katika bidhaa.
Baadhi ya waliohudhulia semina wakifuatilia maada mbalimbali wakati semina hiyo ya kuwajengea uwezo wazalishaji wa bidhaa na wafanyabiashara namna ya ufungashaji wa bidhaa na matumizi sahihi ya vipimo katika bidhaa.
Katibu Tawala msaidizi Mkoa wa Dodoma sekta ya uchumi wan ne kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina hiyo ya kuwajengea uwezo wazalishaji wa bidhaa na wafanyabiashara namna ya ufungashaji wa bidhaa na matumizi sahihi ya vipimo katika bidhaa.
…………………………………………………………………………..
Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.
Wakala wa vipimo Tanzania WMA wameanza kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wazalishaji wadogo wadogo namna ya kutumia vipimo sahihi katika ufungashaji wa bidhaa wanazozizalisha ili kukidhi katika masoko ya ndani na Kimataifa kwenye bidhaa zao.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa semina hiyo Kaimu Afisa Mkuu wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Bi. Stella Kahwa amesema lengo la semina hiyo ni kuwawezesha wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa kuwa na uelewa wa vipimo na matumizi sahihi vya bidhaa zao.
Amesema Wakala wa Vipimo Tanzania wanajukumu la kuhakikisha bidhaa zote zinazozalishwa hapa nchini zinakuwa katika vipimo sahihi na thamani halisi ya bidhaa hiyo ambayo pia inaweza kukidhi vigezo vya Kimataifa na hatimaye kushindana na bidhaa nyingine katika masoko mbalimbali.
“Semina hizi tutafanya nchi nzima na sasa tupo Mkoa wa Dodoma lengo letu ni kuhakikisha wazalishaji wetu wadogowadogo na wafanyabiashara kwa ujumla wanafahamu vipimo sahih ili bidhaa wanazozalisha vipimo vyake zikidhi kiwango cha Kimataifa tushindane na wengine Kimataifa” amesema Bi. Stella.
Amesema semina hizo zimelenga wazalishaji wa bidhaa za kufungashwa wanakuwa kutoka wazalishaji wadogo kuwa wa kati kisha kuwa wazalishaji wakubwa waende hadi Kimataifa kwa kuwa wafanyabiashara wakubwa sana.
Amesema Wakala wa Vipimo wanatoa miongozo kwa wazalishaji wa ndani na ambapo wamewataka wafanyabiashara na wazalishaji kufuata miongozo hiyo ili waweze kukidhi matakwa ya Kimataifa ambapo Tanzania ni mwanachama wa shirika la Vipimo Duniani.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Dodoma bwana Karim Zuberi amesema semina hiyo ni mwendelezo wa semina ambazo wamekuwa wakitoa wanapowatembelea wafanyabiashara na wazalishaji mmoja mmoja katika maeneo yao ya kazi ambapo pia wamekuwa wakiwashirikisha watendaji wa kata.
Amesema wamekuwa na utaratibu huo lengo ni kuhakikisha Mkoa wa Dodoma unakuwa na bidhaa zilizokidhi kwa kuwa na uzito sahihi na kutoa onyo kwa wazalishaji na wafanyabiashara wenye tabia ya kuchezea vipimo kuacha mara moja kwa kuwa Sheria ni kali ambapo faini yake uanzia laki moja hadi milioni ishirini kulingana na kosa.
Kwa upande wake Katibu tawala msaidizi Mkoa wa Dodoma Sekta ya Uchumi Bi. Aziza Mumba aliyekuwa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema sekta ya vipimo ni nyeti sana kwa uzalishaji wa bidhaa hasa katika kipindi hiki kumekuwa na hamasa kubwa ya uanzishwaji wa viwanda ambapo kwa Mkoa wa Dodoma viwanda zaidi ya elfu tatu vilianzishwa.
Amebainisha kuwa semina hiyo itakuwa chachu kubwa ya uzingativu wa vipimo sahihi vya bidhaa katika bidhaa mbalimbali kwani awali walikuwa wakipokea malalamiko mengi kwa wananchi kutokupata vipimo sahihi vinavyotakiwa katika bidhaa wanazozinunua.
Amesema kuna haja ya mamlaka za serikali za mitaa kutilia mkazo vipimo sahihi katika minada kwani kuna baadhi ya minada hawatumii vipimo sahihi katika bidhaa mbalimbali hasa katika mifugo mara nyingi wamekuwa wakikadiria ukubwa wa mnyama ambapo huwezi kupata thamani halisi ya mifugo.
Naye mmoja wa waliohudhuria semina hiyo Bi. Merry Barnabas ambaye anatoka katika kikundi cha wanawake wapambanaji ambao wanazalisha bidhaa mbalimbali amesema semina hiyo itakuwa msaada mkubwa kwao kwani sasa wamejua matumizi ya vipimo sahihi.
“Semina hii ni nzuri naamini tukitoka hapa tutakuwa katika hatua nyingine na tumeona kuna haja ya kutumia vipimo sahihi katika bidhaa zetu bila kuwaibia wateja wetu kutipia vipimo jambo ambalo hata Mungu hapendi” amesema Merry.