Home Mchanganyiko Timu za Uendeshaji na Usimamizi wa huduma za afya Mkoa na Halmashauri...

Timu za Uendeshaji na Usimamizi wa huduma za afya Mkoa na Halmashauri zashauriwa kusimamia utekelezaji wa afua za afya

0

******************************

Na Angela Msimbira KILIMANJARO

Timu za Uendeshaji na Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa na Halmashauri kwa kushirikiana na Maafisa Maendeleo wa Jamii Mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha jamii inashirikishwa katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ikiwemo miradi ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya ili kupunguza gharama za ujenzi na kuongeza umiliki wa miradi hiyo.

Ametoa ushauri huo leo katika kikao kazi kilichohusisha timu ya usimamizi shirikishi ya huduma ya afya kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Timu za Uendeshaji na usimamizi wa Huduma za afya ya Mkoa na Halmashauri,Mkoani Kilimanjaro

Afisa Maendeleo ya Jamii, Ofisi ya Rais –TAMISEMI Bi. Hilda Mgomapayo ameendelea kuzishauri timu hizokuhakikisha wanahamasisha na kutoa elimu kwa jamii kwa kushirikiana na maafisa maendeleo ya Jamii ili kubadilisha mitazamo hasi kuhusu Matumizi ya vyandarua na kuongeza Matumizi ya vyandarua na hatimae kutokomeza malaria..

Amezishauri Timu hizo kuhakikisha zinashirikisha Ofisi za Serikali za vijiji/mitaa na Kata kupata taarifa ya Matumizi ya vyandarua ili kuhakikisha Matumizi sahihi ya vyandarua yanazingatiwa.

Hata hivyo, amewashauri kusimamia utekelezaji wa afua ya upuliziaji wa viuwa dudu katika mazalia ya mbu na kuhakikisha Halmashauri zao zinatenga fedha kwa ajili na kununua dawa ya viuwadudu kwa ili kupulizia malazia ya mmbu.