Home Mchanganyiko IPO HAJA KWA MAMLAKA MBALIMBALI KUTAMBUA NA KUTHAMINI MCHANGO WA UHURU WA...

IPO HAJA KWA MAMLAKA MBALIMBALI KUTAMBUA NA KUTHAMINI MCHANGO WA UHURU WA HABARI

0

Mwandishi wa habari mkongwe Zanzibar Salim Said Salim akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari kwa upande wa Zanzibar.

Mkurugenzi wa TAMWA-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa akifungua kongamano la majadiliano kuhusu rasimu ya sharia ya habari katika madhimisho ya siku ya uhuru wa hahari kwa upande wa  Zanzibar.

******************************

Wakati Dunia leo ikiadhimisha siku ya uhuru wa habari visiwani Zanzibar imelezwa kuwa  ipo haja kwa mamlaka mbali mbali kutambua na kuthamini mchango wa waandishi wa habari  na uhuru wa kupata habari kwa kuwa ni haki ya kikatiba zote mbili za Tanzania.

Hayo yamalezwa katika kongamano la siku moja lililofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara mjini Unguja ambalo washiriki walipsata  nafasi ya kupitia na kujadili rasimu ya sharia ya habari.

Wakati hayo yakijiri  Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa habari wanawake TAMWA-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa alisema upatikanaji wa habari pia unachochea kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Nchi hivyo kuna kila sababu wananchi na wanahabri kupewa uhuru wao wa kufanya kazi bila ya kubugudhiwa.

Pia Mkurugenzi huyo amewataka wanahabari kujikita zaidi katika kujiongezea elimu kwani elimu ndio itakayowasaidia na kuwafanya kuwa wapambanuzi na mambo mbali mbali sambamba na kuepuka changamoto za hapa na pale.

Katika hatua nyengine aligusia pia suala la udhalilishaji wa kijinsia kwa wanahabari wanwake visiwani hapa na kusema iwapo kuna wanahabari wanafanyiwa matendo hayo au kuona viashiria wasikae kimya na wanapaswa kutoa taarifa mamlaka husika.

Kwa upande wake mkuu wa kada ya habari  Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA)Imane Osmond Duwe alisema ipo haja ya wanahabari kufanya kazi zao kwa mujibu wa taaluma na kwa kuwa watafahamu kwa kina nini wanakifanya na wanachokitaka kwa maslahi ya Taifa na jamii kwa ujumla.

Pia alisema dhana ya uhuru wa habari haishii tu kwa waandishi wa habari bali inakwenda hadi kwa jamii ya kawaida kwa vile jamii nayo inapaswa kupata taarifa juu ya yanayoendelea ndani nan je ya Nchi.

Sambamba na hayo alisema alisema kila mtu anapaswa kufahamu kuwa kila aina ya uhuru una mipaka yake hivyo uwepo wa mipaka ya kupata habari isiwe kigenzo cha kuwanyima wanahabari kufanya kazi yao.00000

Kwa upande wake mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salam kitivo cha sharia Profesa  Chris Maina Peter alisema wakati Dunia leo inaadhimisha siku hii ya uhuru wakupata habari kila mmoja anapaswa kufahamu kuwa uhuru wa kupata habari ni miongoni mwa haki za msingi kwa kila binadamu.

Alisema kutoka na msingi huo ndio maana Serikali zote mbili wakaona umuhimu na kuweka kwenye katiba zao haki ya kupata habari hivyo inapotokea mtu ama taasisi kunyima wengine wasipate habari ni kwenda kinyume na katiba zote mbili.

Maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari hufanyika kila mawaka ifikapo mei tatu ambapo kwa mwaka huu ujumbe ni habari kwa manufaa ya umma.