******************************
1.1 MUHTASARI WA MWENENDO WA VIASHIRIA NA MFUMO WA MVUA KWA
TAREHE 21-30 APRILI, 2021.
Kati ya tarehe 21-30 mwezi Aprili 2021, migandamizo mikubwa ya hewa iliyo kaskazini mwa
dunia (Azores na Siberia) iliendelea kudhoofika wakati ile iliyopo sehemu ya kusini mwa dunia
(St. Helena na Mascarene) iliimarika. Ukanda wa mvua (ITCZ) ulielekea kaskazini. Joto la bahari
katika maeneo ya kusini-magharibi mwa bahari ya Hindi lilikuwa la wastani hadi chini kidogo ya
wastani na kusababisha uwepo hafifu wa vimbunga baharini. Upepo ulivuma kutoka kaskazini
mashariki hadi mashariki katika maeneo ya kaskazini mwa nchi na kutoka kusini mashariki hadi
mashariki katika maeneo ya kusini mwa nchi hali iliyoashiria kuimarika kwa ukanda wa mvua wa
ITCZ. Eneo la Kusini-mashariki mwa bahari ya Atlantiki (karibu na pwani ya Angola) kuliendelea
kuwepo na joto la bahari la wastani hadi juu kidogo ya wastani. Hali hii ilisababibisha kupunguza
mchango wa mifumo ya kusababisha mvua katika maeneo ya magharibi mwa nchi.
1.2 MUHTASARI WA MWENENDO WA MVUA KWA TAREHE 21-30 APRILI, 2021.
Mwenendo wa viashiria vya hali ya hewa hapo juu vinaonyesha uwepo wa ukanda wa mvua wa
ITCZ uliopelekea vipindi vya mvua zilizoambatana na ngurumo za radi katika maeneo ya ukanda
wa ziwa Viktoria, nyanda za juu kaskazini mashariki, Pwani ya kaskazini na magharibi mwa nchi
na vipindi vichache vya mvua zilizoambatana na ngurumo za radi katika maeneo ya kati mwa nchi.
Mvua nyepesi katika maeneo yaliyosalia.
2.0 MATARAJIO YA HALI YA HEWA KWA TAREHE 01- 10 MEI, 2021.
2.1 VIASHIRIA NA MFUMO WA MVUA KWA TAREHE 01- 10 MEI, 2021
Katika kipindi hiki, migandamizo mikubwa iliyopo kaskazini mwa dunia (Azore na Siberia)
inatarajiwa kuendelea kudhoofika wakati ile iliyopo kusini (St. Helena na Mascarene) inatarajiwa
kuendelea kuimarika. Ukanda wa mvua (ITCZ) unatarajiwa kuendelea kusogea taratibu kuelekea
kaskazini mwa nchi. Joto la bahari la wastani linatarajiwa katika eneo la kusini-magharibi mwa
bahari ya Hindi hali inayopunguza uwezekano wa kutokea vimbunga katika bahari. Upepo
unatarajiwa kuvuma kutoka kusini mashariki hadi mashariki katika maeneo yote ya Pwani ambao
utasababisha kuwepo na vipindi vya mvua katika nusu ya kwanza ya dekadi. Eneo la Kusini-
Page 2 of 2
Kwa Mawasiliano:
Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Ubungo Plaza, Ghorofa ya 3, 388 Morogoro Rd
S. L. P. 3056, 16102 Dar es Salaam, Tanzania. Nukushi: +255 22 2460735, Simu: +255 22 2460706-8
Barua pepe: [email protected], Tovuti: www.meteo.go.tz
727F –00/2019
mashariki mwa bahari ya Atlantiki (karibu na pwani ya Angola) kunatarajiwa kuwa na joto la
bahari la wastani hadi juu kidogo ya wastani. Hali hii itapelekea kupunguza kasi ya upepo uvumao
kutoka magharibi hivyo kupunguza nguvu ya mifumo isababishayo mvua katika maeneo ya
magharibi mwa nchi.
2.2 MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 01- 10 MEI, 2021.
Kanda ya ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara):
Vipindi vya mvua vitakavyoambatana na ngurumo za radi katika baadhi ya maeneo.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro,): Vipindi
vya mvua vitakavyoambatana na ngurumo za radi katika maeneo machache.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar
es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vya mvua vitakavyoambatana na
ngurumo za radi katika baadhi ya maeneo.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Vipindi vya mvua
zitakazoambatana na ngurumo za radi katika maeneo machache.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Vipindi vya mvua nyepesi katika maeneo
machache.
Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa):
Vipindi vya mvua nyepesi katika maeneo machache.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Vipindi vya mvua nyepesi katika maeneo
machache.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Vipindi vya mvua
nyepesi katika maeneo machache.
Imetolewana; MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA