Mkutano wa wadau wa kupokea
maoni ya kanuni za wakala wa Meli na Forodha ukiandelea kwenye Ukumbi wa Bandari Jijini Tanga leo
Wadau wakifuatilia mkutano wa wadau wa kupokea
maoni ya kanuni za wakala wa Meli na Forodha leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Bandari Jijini Tanga
Wadau wakifuatilia kwa umakini mkutano wa wadau wa kupokea
maoni ya kanuni za wakala wa Meli na Forodha leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Bandari Jijini Tanga
MKUTANO wa Wadau wa kupokea maoni ya kanuni za Wakala wa
Meli na Forodha umefanyika leo mkoani Tanga ukihusisha wadau wa usafi kwa njia
ya maji ikiwemo Bahari na Maziwa ambao ulijadili mapendekezo ya kanuni mpya za
watendakazi wanaosimamiwa na Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC).
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wake ambae ni
Mkurugenzi wa Mazingira na Usalama katika Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na
hususani Idara ya Usafiri wa Usalama wa Mazingira ya Usafiri nchini Stella
Katondo ambapo alisema wamewakutanisha wadau hao ili kujadili mapendekezo ya
kanuni mpya katika kuanzisha kanuni za Benchmark za wale watenda kazi wanaosimamiwa
na Shirika la TASAC.
Alisema kwamba wanataka wawe na vigezo vya upimaji watendaji
kazi wao na wamepeleka mapendekezo hayo na watayapokea maoni kutoka kwao ambao
wanashiriki kwenye kazi hizo ili waweze kuyaweka kwenye kanuni ili pale
wanapofanya kazi waweze kuwa wamepimwa watatekeleza kazi hizo hasa kule chini
kwa walaji ambao watakuwa wanapata huduma ambazo wanazitoa.
Aliwataja watendaji hao ni Wakala wa Forodha,Clearing and
Forwarders na wenye meli na wote wanaohusika kwenye tasnia hiyo ili kuweza
kuanzisha hizo kanuni ambazo
zitawasaidia wakati wanapokuwa wakitumiza wajibu wao.
“Kumekuwa na mapendekezo ya marekebisho kwenye kanunuzi hizo
kanuni zilikuwa tayari hivyo hivi sasa tunatarajia kuzirekebisha ziendane ma
mazingira yatakayohusisha upamaji wa utendaji kwa ufupi ni hivyo tupo mkoani
Tanga kwa ajili ya kuendelea kupata maoni kwa wadau”Alisema
Alisema vikao kama hivyo vinafanyika leo Mkoani Mwanza na Tanga na Mei 5 mwaka huu mkutano huo utafanyika Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo wa Mazingira na Usalama Uchukuzi alisema japo kumekuwa na ushirikishwaji kwenye maeneo
ya maziwa makuu walikuwa hawajashirikishwa katika zile kanuni za awali kwa
kwenye mapendekezo hayo mapya.
“ Hivyo ndio maana leo kwenye vikao vya wadau vinaendelea
Mwanza kwa kuwashirikisha wadau maeneo
hayo kwani Shirikia la Meli sio linafanya kazi kwenye mwambao wa bahari tu bali
hata kusimamia watendaji kazi waliopo kwenye maziwa makuu”Alisema
Ambayo yanaendesha huduma za usafirishaji kwa njia ya maji
kwa meli hicho ni kipengele ambacho kimekumbukwa na kimepelekwa kwa wadau
kusubiri waweze kutoa mapendekezo yao ili kuiingizwe katika kanuni ambazo
zinatarajia kusimamia utendaji kazi.
“Katika kanuni hizo wametoa nafasi kwa wadau kwanza waweze
kutoa mapendekezo na hatimaye kiingizwe kwenye kanuni,wamepewa nafasi kwanza
wadau wamepeleka mapendezo yao yatapokelewa na sekratarieti kwani ni mchakato
hivyo bado wana nafasi ya kupokea maoni.
Awali akizungumza katika mkutano huo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nason Sigala alisema kinachofanyika
katika mkutano huo ni ukusanyaji wa kupokea maoni kutoka kwa watumiaji,wadau
katika sekta ya usafiri na usafirishaji wa majini.
Alisema zoezi hilo la upokeaji wa maoni ya mapendekezo ya
kanuni mpya za vigezo vya utendaji na marejeo ya marekebisho ya kanuni ya wakala
wa mali ni mchakato ambao unataratibiwa na wizara ya Ujenzi na Uchukuzi sehemu
ya uchukuzi.
Sigalla ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa TASAC
alisema wao kama Shirika la Wakala wa Meli Tanzania(TASAC) wameshiriki kwenye
vikao hivyo kama wadau muhimu baada ya kanunu hizo kupitishwa wao watahusika
moja kwa moja kama msimamizi katika utekelezaji hivyo matarajio yao baada ya
kanunuzi hizo kupiti kwa kiasi kikubwa ufanisi na ubora wa huduma
zinazodhibitiwa utaimarika kwa kiwango kikubwa.
Naye kwa upande wake mmoja washiriki kwenye mkutano huo
kutoka Kampuni ya CMA Shiping Line Lucy Jackson alisema marekebisho ya kanuni
ambazo wameelezewa vitawasaidia wadau wanaotumia bandari kunufaika kwa sababu
zimefanyiwa marekebisho na kukidhi mahitaji ya wateja.
Lucy alisema kabla ya kununi hizo kupendekeza zilikuwa
zinawaathiri katika utendaji wa kazi nyakati tofauti tofauti kwa sababu unakuta kanuni
hazijabezi kwa watumaji wa bandari kwa hiyo marekebisho yameangalia ni athari
gani walikuwa wanazipata.
Alisema baada ya marekebisho hayo wanategemea watanufaika
huku akieleza kwamba ilikuwa inawaadhiri kwa upande wa Shiping Line kwa sababu unakuta
wateja wao ambao ni wadau wakubwa wanaohusiana na makasha hawajui hizo sheria hivyo namna ya kuwaelezea
inakuwa vigumu.