Afisa Ufuatiliaji wa TASAFkutoka makao makuu Dodoma Bw Salum Mshana akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Ukuli, Kata ya Kingerikiti Wilayani Nyasa katika Mkutano wa Kijiji wa Kuteua wanufaika wa Mpango wa TASAF awamu ya pili Wilayani hapa.Picha na Ofisi ya Ded Nyasa
**********************************
Afisa Ufuatiliaji kutoka makao makuu ya TASAF Bw. Salumu Mshana amewataka wananchi wa Wilaya ya Nyasa kushirikiana ili kuwapata wanufaika Mpango wa TASAF.
Ameyasema hayo hivi karibuni wakati akifanya ufuatiliaji wa uibuaji wa wanufaika wa mpango wa TASAF wakati wa mikutano ya Hadhara iliyofanyika katika Kijiji cha Ukuli Kata ya Kingerikiti na Kijiji cha Luhangarasi Kata ya Luhangarasi Wilayani Nyasa akiwa anafuatilia jinsi zoezi la uibuaji linavyoendelea.
Bw. Mshana amefafanua kuwa amelazimika kufanya ufuatiliaji ikiwa ni jukumu lake la kuhamasisha jamii na aweze kuona kwa macho jamii inahusikaje kuandaa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini kipindi cha pili TASAF ili uweze kufanikiwa kwa kuwapata wanufaika wakidhi vigezo.
Ameongeza kuwa Tayari mafunzo yametolewa kwa viongozi wa Wilaya na wawezeshaji ngazi ya jamii na wako katika vijiji vyetu 32 ambavyo awali havkuwa katika mpango.hivyo mameitaka jamii kuhudhuria katika mikutano inayoitishwa na viongozi wao na kuwaibua walengwa waliokidhi vigezo.Ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu zoezi hilo ili liweze kukamilika kwa ufasaha.
“Nichukue fursa hii kuwaomba mshiriki kikamilifu kuwaibua wanufaika wanaostahili kwa kuwa mpango huu umeanza muda mrefu na umepitia changamoto mbalimbali sasa tunawataka wananchi wote mjitokeze kwa wingi katika mikutano ya kuwaibua wanufaika ili tuwapate kwa vigezo vya kitaifa na vigezo ambavyo wamepewa na wawezeshaji.
Aidha, amepongeza kwa kujitokeza kwa wingi katika mikutano na kuwaomba waendelee na mchakato mpaka ukamilike kwa kufuata utaratibu waliojiwekea kwa kushirikiana na wawezeshaji ambao wamepewa mafunzo kwa ajili ya kutekeleza zoezi la utambuzi wa wanufaika hao.