**********************************
Na. Mwandishi wetu, Tanga
Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) imesema kuwa ni muhimu sana Jamii kushirikishwa katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ikiwemo miradi ya ujenzi wa vituo vya afya na zahanati.
Kauli hiyo imebainishwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Hilda Mgomapayo ,kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi na Timu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Huduma ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli.
Bi. Mgomapayo ameeleza kuwa ushirikishwji wa jamii unatoa fursa kwa Jamii kushiriki kwa kuchangia nguvu kazi ikiwa Ni pamoja na kuchimba msingi, kukusanya mawe, kusomba mchanga na hata kuchangia fedha inapobidi.
“Hii hupunguza garama na ujenzi na hivyo kufanikisha mradi kukamilika na pia ina leta ‘ownership’ ya mradi na kufanya usimamizi kikamilifu”, ameeleza Bi.Mgomapayo.
Aidha ametoa wito kwa watoa huduma za afya kushirikiana na maafisa mafisa maendeleo ya Jamii ili kuhakikisha wanafanya Uhamasishaji wa wananchi kujiunga na bima ya afya ya Jamii iliyoboreshwa (ICHF).
Bi. Mgomapayo ameongeza kuwa HALMASHAURI ya Bumbuli iko chini Sana katika usajili wa wanachama wa ICHF kwani kutokana na taarifa ya mpaka kufikia mwezi jana April 2021 imesajili kwa 0.6%.
“Uhamasishaji ufanyike kwa kushirikiana na maafisa maendeleo ya Jamii ambao Wana weredi katika kuraghibisha, kuhamasisha na kufanya uchechemuzi kwa Jamii ili kuongeza usajili katika Halmashauri ya Bumbuli”, amesisitiza Bi. Mgomapayo.
Hata hivyo amesema kuwa kuna malalamiko ya wananchi baadhi ya maeneo kuandikishwa lakini majina yao hayaonekani kwenye mfumo , hivyo amegiza mratibu wa ICHF kwa.kushirikiana na CHMT kuhakikisha wananchi wote waliosajiliwaqanonekana kwenye mfumo na kupata huduma stahiki.
Katika upande mwingine Bi. Mgomapayo amesema CHMT wanapokwenda kwenye ufuatiliaji katika vituo watembelee katika Ofisi za Serikali za Kata na vijiji ili kupata taarifa ya Matumizi ya vyandarua ili kuhakikisha Matumizi sahihi ya vyandarua yanazingatiwa.
Serikali unatumia pesa nyingi Sana kwa ajili ya kugharimia vyandarua vyenye dawa kwa ajili ya kugawia wananchi. Kuna baadhi ya maeneo vyandarua vina tumika kwa kufugia vifaranga, kuvulia samaki na kufunikia bustani. Kama hakutakuwa na Matumizi sahihi ya vyandarua, lengo la Serikali la kutokomeza malaria ifikapo 2030 halitafikiwa.
Vile vile ametaka uhamasishaji na elimu iendelee kutolewa kwa kushirikiana na maafisa maendeleo ya Jamii ili kubadilisha mitazamo hasi ya Jamii kuhusu Matumizi ya vyandarua ili kuongeza Matumizi ya vyandarua na hatimae kutokomeza malaria.