*****************************
Na. Mwandishi wetu, Tanga
Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Hilda Mgomapayo, kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), amezitaka timu ya uendeshaji na usimamizi wa huduma za afya za Halmashauri (CHMT) kuendelea kusimamia utekelezaji wa Propram ya WASH kwa kuhakikisha vituo vya kutolea huduma za afya vinakuwa na vifaa vya kunawa mikono pamoja na sabuni ili kuzuia magonjwa mbali mbali.
Wito huo umetolewa leo katika kikao kazi na Timu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Huduma ya Afya katika Halmashauri ya Lushoto, mkoani Tanga.
Bi. Mgomapayo Ameongeza kw kusema kuwa, katika Jamii pia kunatakiwa kuwa na vyoo Bora na kuhimiza Matumizi ya vyoo, usafi wa vyoo, Matumizi ya maji ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni.
“Pamoja na kuhimiza utoaji wa huduma Bora kwa wananchi CHMT inapaswa kusimamia usalama mahala pa kazi kwa watoa huduma ili kuhakikisha watumishi wanapata stahiki zao ili kuwapa motisha katika kazi”, amesisitiza Bi.Mgomapayo.
Kuwa Mazingira mahala pa kazi yaangaliwe na pia kuwajengea uwezo wa kuandaa mpango kazi ambo unalenga kuboresha mazingira yao ya kazi ikiwa Ni pamoja na kununua samani Kama vile viti, meza, makabati na kadhalika ili kuingiza katika Bajeti zao.
Aidha Bi.Mgomapayo amesema kuwa DMO, Mratibu wa ICHF pamoja na CHMT kuhakikisha wanachama wote ambao wamelipia elfu 30 kwa ajili ya ICHF na hawajaingizwa kwenye mfumo waingizwe ndani ya siku 14.
“Ni kosa kwa mwanachama kulipia na kutoingizwa kwenye mfumo kwani inasababisha kukosa huduma wakati wamelipia fedha. Hii inapelekea wananchi kuvunjika moyo na kutojisajili na hivyo kusababisha usajili kuwa chini”, ameeleza Bi.Mgomapayo.
Lakini pia Michango ya wananchi ambayo inatolewa kwa ajili ya kuchangia miradi ya maendeleo Kama vile mchanga , mawe, nguvu kazi kwa kuchimba msingi, mashimo ya vyoo , kufyatua tofali vithaminishwe kwa thamani ya fedha ili kujuwa mchango halisi wa wananchi katika miradi hiyo.
Bi.Mgomapayo ameeleza kuwa jambo hilo linatoa motisha kwa Jamii na kusaidia kujuwa thamani halisi ya miradi na pia kudhibiti ubadhilifu kwa watu wasio waaminifu.