Home Michezo MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED WALETA VURUGU, WASHINIKIZA FAMILIA YA GLAZER KUACHIA TIMU

MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED WALETA VURUGU, WASHINIKIZA FAMILIA YA GLAZER KUACHIA TIMU

0

**************************

NA EMMANUEL MBATILO

Maelfu ya Mashabiki wa klabu ya Manchester United wamejitokeza kwa wingi uwanjani Old Traford na nje ya uwanja kushinikiza familia ya Glazer kuiachia timu hiyo na kupelekea mechi ambayo ilikuwa ichezwe leo saa 12:30 jioni kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool kuhairishwa.

Polisi wameingilia kati na kutuliza ghasia lakini inavyoonekana wafuasi wa Manchester united ni wengi hivyo uongozi wa ligi ukaamua kuisimamisha mechi hiyo kwaajili ya usalama.