Katibu Tawala msaidizi Mkoa wa Arusha anayeshughulika na sekta za kiuchumi na uzalishaji mali Agney Chitukuro akifunaga kikao kazi hicho.
Kaimu Mkurugenzi huduma za biashara kutoka TANTRADE Makao Makuu,Twuilumba Mlelwa akiongea katika kikao kazi hicho
Washiriki wa kikao kazi cha Tantrade kilichofanyika mkoani Arusha hivi karibuni.
……………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (TANTRADE) ipo kwenye mchakato wa kuandaa muongozo maalum utakaowawezesha wadau wote wanaosimamia sekta ya biashara kuwa na mfumo utakaowasaidia kukusanya, kuchakata na kusambaza taarifa za biashara kwa wakati.
Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi huduma za biashara kutoka TANTRADE Makao Makuu,Twuilumba Mlelwa katika kikao kazi kilichofanyika mkoani Arusha ambapo amesema kuwa taarifa za biahara ni kiungo muhimu kitakachowawezesha wazalishaji na wa wafanyabiashara kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati muhafaka juu ya masuala yanayohisiana na biashara.
“Baada ya kikao kazi hiki pia tuataendelea kukusanya maoni katika mikoa mbalimbali ambapo kwa awamu ya kwanza tunakusanya Arusha, Dar es salaam, Mwanza, Mtwara, Mbeya, Songwe pamoja na Zanzibar na baada ya kukusanya maoni yote yatatuwezesha sasa kuwa na mfumo shirikishi ambao utatuwezesha kufika katika mikoa mingine ambayo kwasasa haijaweza kupitiwa, Alisema Twailumba.
Alifafanua kuwa matarajio yao kwa nchi nzima ni kuweza kuwa na mfumo utakaowawezesha kutambua bei mbalimbali za bidhaa za kilimo, uvuvi, mifugo pamoja na misitu katika jukwaa moja ili ziweze kusambazwa wa wazalishaji wa bidhaa hizo, wananuzi na wadau wengine wanaofanya tafiti na ushauri wa masuala mbalimbali ya kisera.
Pia alitoa wito kwa maafisa biashara pamoja na maafisa wanaosimamia sekta hizo hasa wanaosimamia masoko kuendelea kushirikiana katika kuwahudumia wafanyabiashara mbalimbali na kuhakikisha kwamba taarifa zinazopatikana wanazisambaza kwa wakati ili ziwe na manufaa kwa wadau wa biashara.
Kwa uapande wake Katibu Tawala msaidizi Mkoa wa Arusha anayeshughulika na sekta za kiuchumi na uzalishaji mali Agney Chitukuro akifunaga kikao kazi hichi aliwataka maafisa biashara ngazi za wilaya na mkoa kutumia muongozo huo utakapatikana katika kukusanya,kuchakata na kusambaza taarifa ili kuweza kupata takwimu sahihi zinazohusu biashara.
Chitukuro alisema kuwa mfumo huo utasaidia kuondoa tatizo katika ukusanyaji wa takwimu sahihi na kuzichakata taarifa ambapo kama serikali watatoa ushirikiano wa asilimia 100 kama muongozo huo ukikamilika kwa kuupokea na kwenda kuufanyia kazi.
“Arusha ni miongoni mwa mikoa ambayo masuala ya biashara yameshamiri kwahiyo tunaamini kuwa muongozo huu ukikamilika na kuwa na mfumo huo utakuwa na tija kubwa kwa wazalishaji na wafanyabiasha wa mkoa huu,” Alisema Chitukuro.
Naye mmoja wa washiriki katika mafunzo hayo Pius Rimoy Afisa biashara kutoka halmashauri ya Meru alieleza kuwa mfumo huo utawasaidia kujua ni jinsi gani taarifa zitaweza kupatikana lea usahihu kuhusiana na masuala ya uzalishaji na ununuzi.
Hata hivyo mafunzo hayo yalihusisha maafisa biashara,maafisa wanaosimamina Sekta za kilimo,mifugo,uvuvi pamoja na wadau wengine wa biashara hususani wale wanaosimamia masoko mbalimbali kutoka ndani ya mkoa wa Arusha.