KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dk. John, akikagua Mabanda wakati akifunga mkutano wa mwaka wa wadau wanaotekeleza afua za VVU na Ukimwi zinazowalenga wasichana balehe na wanawake vijana uliomaliza leo April 30,2021 jijini Dodoma baada ya kufanyika kwa siku mbili.
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dk. John, akitoa hotuba wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa wadau wanaotekeleza afua za VVU na Ukimwi zinazowalenga wasichana balehe na wanawake vijana uliomaliza leo April 30,2021 jijini Dodoma baada ya kufanyika kwa siku mbili.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dk. John, wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa wadau wanaotekeleza afua za VVU na Ukimwi zinazowalenga wasichana balehe na wanawake vijana uliomaliza leo April 30,2021 jijini Dodoma baada ya kufanyika kwa siku mbili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk.Leonard Maboko,akizungumza wakati wa kufunga Mkutano wa Mwaka wa wadau wanaotekeleza afua za VVU na Ukimwi zinazowalenga wasichana balehe na wanawake vijana uliomaliza leo April 30,2021 jijini Dodoma baada ya kufanyika kwa siku mbili.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dk. John, akiwa katika picha mara baada ya kufunga Mkutano wa Mwaka wa wadau wanaotekeleza afua za VVU na Ukimwi zinazowalenga wasichana balehe na wanawake vijana uliomaliza leo April 30,2021 jijini Dodoma baada ya kufanyika kwa siku mbili.
………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dk. John Jingu, amewataka Wasichana kujitambua,kujiamini,kukataa vishawishi na marafiki wabaya ili kuweza kutimiza ndoto zao walizojiwekea.
Kauli hiyo ameitoa leo April 30,2021 jijini Dodoma wakati akifunga mkutano wa mwaka wa wadau wanaotekeleza afua za VVU na Ukimwi zinazowalenga wasichana balehe na wanawake vijana.
Dk.Jingu amewataka vijana kujitambua na kujiamini kwani ni nyenzo muhimu katika kutatua Changamoto zinazoendana na umri wao.
“Naomba wasichana mjitambue na kujiamini kwani ndiyo nyezo muhimu ya kupambana na changamoto zinazoendana na umri wanu pia mkatae marafiki wabaya”amesema Dkt.Jingu
“Anakuja Sponser anakuimbia nyimbo zote na wewe unaingia mkenge unapata maambukizi ya Ukimwi unapata mimba niambie maisha yatakuwa sawa hapo? ila
ukijitambua hautakubali kudanganyika na mjiheshimu.
Hata hivyo Dkt.Jingu amezitaka shule na vyuo nchini kuanzisha madawati ya jinsia ili yatumike kutoa taarifa na kuwasisitiza vijana wajiepushe na papara za maisha ili kuzifikia ndoto zao, huku taasisi za kiraia akizitaka kuendelea kulisaidia kundi hilo.
“Niwaombe katika vyuo na shule kuwajengea uwezo hawa vijana ili kukabiliana na hizi changamoto,pia mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali na Taasisi mbalimbali tuendelee kulilinda na kulisaidia kundi hili ”amesema Dkt.Jingu
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk.Leonard Maboko amesema kuwa kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2017 unaonesha maambukizi mapya ya VVU asilimia 40 ni vijana wenye umri wa miaka 15-24 huku asilimia 80 wakiwa ni wasichana balehe na wanawake vijana.
“Kwa lugha rahisi katika watu 10 basi wanne ni vijana,tusipochukua tahadhari tutaendelea kuzalisha maambukizi mapya.Ukichukua kundi la vijana ile asilimia 40 basi asilimia 80 ni wanawake,sasa tusiboziba ufa tutajenga ukuta”amesema.
Dkt.Maboko amesema kuwa kuna miradi mikubwa mitatu ambayo inatekelezwa ambayo ni timiza malengo,Drems,Vijana salama ambapo amedai jumla ya Mikoa 13 imefikiwa na miradi hiyo.
“Jumla ya Mikoa 13 ndio ambayo inapata katika Mikoa 16 na sio katika Halmashauri zote zinakuwa zinachukuliwa,”amesema.
Awali Mnufaika wa miradi hiyo,Mariamu Mathias ameiomba Serikali iwasaidie vikundi vya wasichana balehe na wanawake vijana waweze kupewa kipaumbele katika mikopo inayotolewa katika Halmashauri.
“Ombi letu itusaidie vikundi vyetu vipewe kipaumbele Cha mikopo ya 4-4-2 katika Halmashauri,Serikali itutafutie wadau,”amesema.