………………………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Wahitimu 204 waliohitimu ualimu wa elimu maalum ngazi ya Stashahada na Astashahada katika chuo cha ualimu elimu maalum Patandi wameiomba serikali kutoa ajira kwa walimu tarajali ili kupunguza changamoto ya uhaba wa walimu hao mashuleni.
Ombi hilo limetolewa na baadhi ya wahitimu hao katika mahafali ya 24 ya chuo hicho ambapo walisema kuwa pamoja muamko mkubwa iliyopo hivi sasa ya walimu kusomea elimu maalum bado kuna changamoto yaajira kwa walimu wapya pamoja na walimu kazini kutopangiwa vituo vipya vya kazin kutokana na kozi waliyosomewa.
mmoja wa wahitimu hao Fadhili Ashim alisema kuwa wakipata ajira kwa haraka wataweza kwenda kuwasaidia watoto walio katika changamoto mbalimbali za ulemavu wa ikiwemo uziwi, uoni, usonji na ulemavu wa akili hivyo wameiomba serikali kuwapa ajira.
Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Lucian Segesela tofauti na walimu 204 waliohitimu kuna walimu wa mwaka wa kwanza 178 ambao wapo wanasubiri ajira pamoja na kwamba mashuleni kuna uhaba wa walimu hao.
“Niiombe serikali kuwapa kipaumbele walimu hawa ili wakazibe pengo la uchache wa walimu wa elimu maalum lakini pia niwaombe walimu hawa kuwa wakati wakiendelea kusubiri ajira wakaanze kujitolea kwenye shule mbalimbali zenye uhitaji ambapo hii itawafanya kusaidia jamii lakini pia kuongeza uzoefu,” Alisema Segesela.
Sambamba na hayo katika risala ya wahitimu waliahinisha changamoto zingine ikiwemo serikali kutokuboresha maslahi yawalimu wa elimu maalum ambapo wanapohitimu na kurudi vituoni hakuna motisha, uhaba wa vyumba vya madarasa, utoaji wa mafunzo ngazi ya cheri kwa walimu kazini ambao tayari wana vyeti,ukosefu wa ukumbi wa mikutano, ukosefu wa meza na viti katika bwalo, kutokamailika kwa jengo la utawala na mengineyo.
Naye Meneja wa Benki ya NMB tawi la Clock Tower Emmanuel Kishosha ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika mahafali hayo ambapo Bank hiyo iliombwa kusaidia viti na meza katika bwalo la chakula, generetq kubwa I’ll kutatua changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara alisema kuwa kama Benki hiyo imekuwa ikijitahidi kusaidia elimu kwa kutoa gawio linalopelekwa kwenye elimu na wakati mwingine majanga ambapo atapeleka suala hilo kwenye uongozi ili kuona kama wataweza kusaidia jambo hilo.
Kishosha pia alisema kuwakama wadau wore wakishirikiana wataweza kutatua changamoto zinazoikabili chuo hicho na kufanya mazingira kuwa rafiki kwa walimu hao jambo litakalopelekea kuwasaidia watoto watoto wenye mahitaji maalum katika jamii.