………………………………………………………………………………..
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka watu wanaopata msamaha wa vifungo kutoka gerezani kuacha kujihusisha na uvunjifu wa amani ikiwa pamoja na kuacha kujiingiza tena kwenye matukio ya uhalifu na badala yake wajikite katika kuleta maendeleo kwenye jamii.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizindua kitabu cha muongozo wa kufichua na kuzuia uhalifu kitabu ambacho kinalenga kutoa dira hasa katika utekelezaji wa mpango wa Polisi kata kupitia mpango mkakati wa ushirikishwaji wa jamii.
Akimkaribisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kwa ajili ya kuzindua kitabu hicho, msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime amesema kuwa, hadi sasa tayari vitabu 7200 vimechapishwa huku kitabu hicho kikiwa na sura sita ikiwa ni mpango mkakati wa ushirikishwaji wa jamii kwa njia ya elimu katika ngazi ya Kata,Shehia, mtaa na vijiji.
Wakati huo huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amefanya mkutano kwa njia ya mtandao yaani video conference na Bw. Jurgen Stock, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Polisi wa Kimataifa yaani Interpol lenye Makao Makuu yake mjini Lyon nchini Ufaransa, ambapo kupitia mkutano huo mambo mbalimbali kuhusiana na masuala ya kiusalama yamejadiliwa.