…………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi ameupongeza mpango wa ujenzi wa jengo la huduma za nje {OPD} litakalokidhi mahitaji ya watanzania na wageni hasa watalii kwa kuwa na huduma za afya za kimatafa ikiwemo Helkopta za wagonjwa kutua juu yajengo hilo.
Kenana ametoa pongezi hizo wakati alipotembelea jengo la mama na mtoto katika hositali hiyo ambapo alipata fursa ya kuelezewa juu ya mradi wa jengo hilo ambalo litaweza kutatua changamoto nyingi za idara ya afya ikiwemo watalii kupata matibabu.
Aliita halnashauri ya jiji hilokuhakikisha wanatoa fedha za ujenzi wa jengohilo kwa wakati ili liweze kujenga kwa haraka na kutatua changamoto zilizopo ikiwemo ya watalii wanaoingia nchini kufuata matibabu nje ya nchi wanapokutana na changamoto za kiafya wanapokuwa katika vivutio vilivyopo hapa nchini.
“Lakini pia madaktari na wauguzi ambao mpo atika hosipitali nawaasa muwe na lugha nzurikwa wagonja, msibaguanebali fanyeni kazi kwa upendo, umojana mshikamano na kwa kufanya hivi mtaweza kufikia lengo la hosipitali hii la kutoa huduma za afya zilizo bora kwa wananchi na wageni ,”Alisema Kenan.
Kwa upande wake mganga mkuu wa jiji la Arusha Dkt Herry Kagya alisema kuwa jengo hilo litakuwa na idara 14 ndani yake ambapo michoro imeshakamilikana itatoa huduma za kiwango cha kimataifa kwani wana dhana ya utalii wa kimatibabu na wanaamini dhana hiyo itaweza kusaidia ongezeko la watalii hapa kutokana na kuwana uhakika wa kupata matibabu pale watakapokuwa katika matembezi yao.
“Hosipitali hii ikikamilika itaweza kuwatibu watu zaidi ya laki tano wa jiji la arusha, maeneo mengine pamoja na wageni ambapo hadi sasa makadirio yanaonesha itagharimu shilingi bilioni 13 lakini wataalamu bado wako wanaendelea na hesabu ili kujua idadi kamili ya fedha zitazotumika kujenga jengo hili,” alisema Dkt Kagya.
Aidha alifafanua kuwa hosipitali hiyo itakuwa ikijengwa kwa awamu ambapo hadi sasa jiji la Arusha limeshatenga shilingi bilioni 1 kwaajili ya kuanza kujenga na kila mwaka wa fedha itafanya hivyo ili kukamilisha ujenzi wake.
Naye diwani wa kata ya Engutoto ilipo hosipitali ya jiji Diwani Karimu Moshi alisema kuwa tangu hosipitali hiyo ianze kutoa huduma imekuwa ikitoa huduma nzuri amabapo aliwataka watoa huduma kuendelea kutoa huduma kwa weledi na bidii zaidi.