Dereva wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Sias ambayepia ni Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, S/SGT. Msafiri Katikilo akitoa maelezo ya namna ya kutumia moja ya kifaa cha kuzimia moto (Fire Extinguisher) wakati wa mafunzo ya namna ya kujilinda na majanga ya moto kwa Watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) leo jijini Dodoma.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) wakifuatilia mada wakati wa mafunzo ya namna ya kujilinda na majanga ya moto kwa watumishi wa ofisi hiyo leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu(DAHRM) wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Ndg. Magohu Zonzo akichangia mada wakati wa mafunzo ya namna ya kujilinda na majanga ya moto kwa watumishi wa ofisi hiyo leo jijini Dodoma.
Afisa Uchumi Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Ndg. Emmanuel Msengi akipata ushuhuda wa namna ambavyo kifaa cha kuzimia moto(Fire Extinguisher) kinavyopata ubaridi baada ya kutumika wakati wa mafunzo ya namna ya kujilinda na majanga ya moto kwa watumishi wa ofisi hiyo leo jijini Dodoma.
Dereva wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye pia ni Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, S/SGT. Msafiri Katikilo akitoa maelezo ya awali namna ya kutumia vifaa vya zimamoto kabla ya kuanza mazoezi kwa vitendo wakati wa mafunzo ya namna ya kujilinda na majanga ya moto kwa Watumishi wa hiyo leo jijini Dodom
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu (DAHRM) wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Ndg. Magohu Zonzo akifanya zoezi la kuzima moto kwa kutumia Fire Extinguisher(CO2) wakati wa mafunzo ya namna ya kujilinda na majanga ya moto kwa watumishi wa ofisi hiyo leo jijini Dodoma.
Mkaguzi wa Ndani wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Ndg. Peter Lyimo akifanya zoezi la kuzima moto kwa kutumia Fire Extinguisher (Powder) wakati wa mafunzo ya namna ya kujilinda na majanga ya moto kwa watumishi wa ofisi hiyo leo jijini Dodoma.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) wakiwa katika mazoezi ya namna ya kutumia vifaa vya zimamoto wakati wa mafunzo ya namna ya kujilinda na majanga ya moto kwa watumishi wa ofisi hiyo leo jijini Dodoma. (Picha na ORPP)