*********************
Na Mwandishi wetu, Kiteto
MBUNGE wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara, Regina Ndege amegawa taulo za kike 505 kwa wasichana wanafunzi wa shule ya Sekondari Engusero Wilayani Kiteto na mipira miwili kwa ajili ya kucheza mpira wa miguu kwa wavulana wa shule hiyo.
Ndege ambaye kitaaluma ni mwalimu ameyasema hayo kwenye ziara yake ya kutembelea Wilaya ya Kiteto ambapo pia alizungumza na Baraza la wanawake wa Jumuiya ya UWT.
Amewaasa wasichana hao wasome kwa bidii kwani changamoto ya taulo za kike watakuwa wameondokana nayo kwa sasa.
Hata hivyo, amewataka wavulana wa shule hiyo kusoma kwa bidii na kushiriki michezo wakati wa mapumziko ndiyo sababu akawapa mipira hiyo miwili ya mpira wa miguu.
“Naahidi kuwa mstari wa mbele kuwasemea zaidi na kuwa mtetezi wa wanafunzi Bungeni katika changamoto mbalimbali zinazowakabili hasa kwenye suala zima la elimu,” amesema Ndege.
Hata hivyo, wanafunzi hao wamemshukuru kwa kuwezesha kuwapa taulo hizo za kike ambazo kwa namna moja au nyingine zitapungusa changamoto ya sodo.
“Taulo hizi zitatusaidia wanafunzi kuendelea na shule kuepuka na kukaa nyumbani na kukosa masomo siku muhimu katika ukuaji huo,” amesema mmoja kati ya mwanafunzi aliyepatiwa taulo.
Kwa upande wao wanafunzi wanafunzi wavulana walishukuru kwa kupatiwa mipira hiyo miwili ambayo watakuwa wanaichezea pindi wakiwa kwenye mapumziko baada ya masomo.