………………………………………………………………………………….
Nteghenjwa Hosseah, Tanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amesema atazifumua Sekretariet za Mikoa endapo hazitatekeleza majukumu yake ipasavyo.
Waziri Ummy ameyasema hayo alipokua akizungumza na Sekretariet ya Mkoa wa Tanga mapema tarehe 26.04.2021 katika Ukumbi wa Ofiso ya Mkuu wa Mkoa Mkpani hapo.
Mhe.Ummy amesema jicho langu la karibu ni Sekretarieti za Mikoa sitaki nianze kupambana na Halmashauri 184 wakati nina watu kwenye Sekretarieti za Mikoa ambao wako karibu kimazingira na kiutendaji na halmashauri hizo ninataka watekeleze majukumu yao ipasavyo na mimi nipate taarifa zote kutoka kwao.
‘Sitaki kuona Sekretarieti za Mikoa ni watu wa ‘kucompile’ taarifa za Halmashauri tu ninataka kuona zinakaa na Halmashauri zao zinawashauri, mnaweka mambo sawa na mnazisimamia ipasavyo katika utekelezaji wa majuku yako ya kila siku’
Aidha aliongeza kuwa ‘Sekretariet ya Mkoa ambayo nitaibani kuwa wataalam wake ni wazembe na hawatekelezi majukumu yao ipasavyo itabidi watupishe tuweke watu watakaochapa kazi kwa weledi na umakini wa hali ya juu huku wakienda na muda.
Hata hivyo Waziri Ummy amezitaka Sekratariet za Mikoa kusimamia ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri zilizoko kwenye Mikoa yao, Matumizi ya Fedha za mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na kupeleka fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo na utoaji wa mikopo ya asilimia kumi huku wakisimamia marejesho ya mikopo hiyo ili izunguke kwa wananchi wengine wafaidike na mikopo hiyo.