Sehemu ya watoto yatima wanaolelewa kwenye Taasisi ya Jaamia wakiwa kwenye picha ya pamoja nyumba ya msaada wa vyakula walivyokabidhiwa
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala wza Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) akizungumza na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho |
Sehemu ya msaada uliotolewa
Sehemu ya msaada uliotolewa
Sehemu ya msaada uliotolewa
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu ametoa sadaka ya futari
kwa taasisi kubwa za Dini Jijini Tanga na Vituo 10 vya Kulea Watoto Yatima na
Makazi ya Wazee Mwanzange ili kuwawezesha kuweza kutimiza nguzo muhimu wa
uislamu wakati huu wa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Tanga (CCM) ametoa msaada huo leo kwa Taasisi za Tamta,Zaharau,Maawal,Shamsul Maarifa,
Rashaad,Nuruhuda Donge,huku vituo vya kulelea yatima ambayo vimenufaika ni
kituo cha Jaamia Til Islamiya,Chumbageni Tupie, Coodwill,Mwakidila,Makorora na
Makazi ya Wazee wa Mwanzange.
Msaada ambao ameutoa ni Sukari Kg
50,Ngano Kg 50,Mafuta ya kula ndoo kubwa,Majani ya Chai Kg 2 ,Tambi Roba
2,Mchele Kg 100 na Maharage kg 100 ambapo vyakula hivyo vitawasaidia katika
kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa ramadhani.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi
vyakula hivyo Waziri Ummy alisema
ameamua kutoka sadaka hiyo ya futari kwa taasisi hizo na vituo vya kulea watoto
yatima na wazee ili kuweza kuwaondole ugumu wa mahitaji hasa kwenye kipindi
hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani.
“Nimeona nitoe sadaka ya futari kwa
Taasisi na vituo vya kulea watoto yatima na Makazi ya Wazee mwezi wa ramadhani
ambao ni wa kufanya toba na mimi kama Mbunge wao nimeona nitoe kile
alichojaliwa kwao”Alisema
Hata hivyo aliwahimiza watu kuendelea
kutoa sadaka kwa watu wenye uhitaji ikiwemo kwenye Taasisi zenye uhitaji mkubwa
ili kuweza kuwapunguzia makali hususani kwenye kipindi hiki cha mwezi Mtukufu
wa ramdani.
Awali akizungumza baada ya kupokea
msaada huo Katibu wa Idara ya Taaluma wa Taasisi ya Maawal Islamic Mohamed
Shabani alimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo wa sadaka ya futari ambao amewapatia
ambao utawasaidia kwenye kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa mwezi wa ramadhani.
Alisema kikubwa wao ni kuhakikisha wanaendelea
kumuombea kwa mwenyezi Mungu amfanyie wepesi kwenye kutekeleza majukumu yake
ikiwemo kuweza kutimiza malengo yake
“Kwa kweli tunamshukuru Waziri Ummy
ambaye pia ni Mbunge wetu wa Tanga kwa msaada huu na tutaendelea kukuombea kwa
mwezi mungu akuongeze na akufungulie Milango kwenye safari yao”Alisema
Naye kwa upande wake -Mwalimu wa
Taasisi ya Jaamia na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtupie Saidi Juma alimshukuru Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Tanga kwa msaada huo wa futari ambao amewapatia huku akieleza
kwamba wataendelea kumuombea mwenyezi Mungu amfanyie wepesi.
Zoezi hilo la ugawaji wa futari kwa
taasisi za dini na vituo vya kulea watoto yatima ikiwemo makazi ya wazee
limekuwa likifanyika kila mwaka