*************************
Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji
Timu ya Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kutoka katika baadhi ya vyuo ,wametembelea mradi mkubwa wa bwawa la kufua umeme la mwalimu Nyerere liliko Rufiji mkoani Pwani ,ili kujifunza na kujionea kazi iliyofanywa na serikali awamu ya tano kipindi cha Hayati Rais Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI.
Akizungumza mara baada kutembelea mradi huo , Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Mbeya HILARY LOOKEN ambao ndio walioandaa ziara hiyo, anasema mbali ya kujifunza kivitendo lakini pia wanasapoti juhudi za serikali awamu ya tano katika kuipeleka Tanzania katika viwango vikubwa vya kiuchumi kwani mradi huo pamoja na faida nyingi utaeza kuwanufaisha watanzania katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhifadhi mazingira.
” Tumeona tuje kujifunza katika mradi huu kwani katika chuo chetu tuna fani mbalimbali zinazotolewa ikiwa ni pamoja na Fani ya uinjinia, hivyo wanafunzi wamejifunza mengi katika mradi, na niseme tu naipongeza serikali kwa kufanya mradi huu mkubwa wa kimkakati ambao utakwenda kutupeleka katika viwango vingine kiuchumi,” Alisema HILLARY LOOKEN , Rais wa Serikali ya Wanafunzi chuo cha Sayansi sayansi na teknolojia cha Mbeya (MUST).
Mradi huu unajengwa na mkandarasi wa kampuni ya Arab Contractor kutoka Misri utagharimu kiasi cha Trilioni 6.5 na unatarajiwa kujengwa kwa kipindi cha miezi kati ya 36 mpaka 42 ya ukamilishaji wa mradi huo.
Kukamilika kwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi, kutaiwezesha Tanzania kuzalisha kiasi kikubwa cha umeme kitachokasaidia kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa uchumi wa viwanda na mradi wa reli ya kisasa, hatua itakayoiwezesha kupiga hatua kubwa za maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wake.
Baadhi ya wanafunzi waliotembelea mradi huo ,waliipongeza serikali kutekeleza Ujenzi huo mkubwa wa kimkakati ambao unakwenda kuwanufaisha watanzania moja kwa moja.
Mhandisi DAVID MUNKALA ni Mtaalamu wa Maji wa Mradi wa Julius Nyerere, alisema Utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme wa maji la Julius Nyerere kwenye bonde la mto Rufiji unaendelea kwa kasi inayohitajika na kuwa unatarajiwa kukamilika kipindi cha mkataba uliosaniwa.