BAO la kujifunga la kipa Mjerumani, Bernd Leno dakika ya 72 jana limeipa Everton ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji, Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates Jijini London.
Kwa ushindi huo, Everton inafikisha pointi 52 baada ya kucheza mechi 32, ingawa inabaki nafasi ya nane, wakati inabaki na pointi zake 46 za mechi 33 sasa katika nafasi ya tisa.