Home Mchanganyiko PROF.OLE GABRIEL AIAGIZA TALIRI KUFANYA TAFITI ZITAKAZOSAIDIA KUPIGA HATUA KUPITIA SEKTA YA...

PROF.OLE GABRIEL AIAGIZA TALIRI KUFANYA TAFITI ZITAKAZOSAIDIA KUPIGA HATUA KUPITIA SEKTA YA MIFUGO

0

……………………………………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

 SERIKALI imetoa maagizo kwa Taasisi ya utafiti wa mifugo Tanzania (TALIRI), kufanya tafiti zitakazo lisaidia taifa kupiga hatua kupitia sekta ya mifugo.

Hayo yamesemwa leo April 23,2021 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel, akizungumza  wakati wa  kikao cha baraza la wafanyakazi wa Taasisi hiyo.

Prof.Ole Gabriel amesema kuwa hakuna taasisi nyingine ambayo wizara hiyo inaweza kuitegemea katika suala la utafiti zaidi ya TALIRI, hivyo ni lazima ifanye tafiti zitakazo boresha sekta ya mifugo nchini na kuchangia pato la taifa.

“Tusibakie kujisifu tuu kuwa Tanzania ni nchi ya pili barani afrika kwa idadi kubwa ya mifugo lazima tujisifie kwa namna tutavyoweza kutumia sekta hii kukuza uchumi wa taifa”amesema Prof.Ole Gabriel

Hata hivyo amesema  kuwa tafiti ndizo zinaweza kulisadia taifa kutoka hapa lilipo na kupiga hatua kufikia nchi ambazo zimefanikiwa katika sekta ya mifugo.

“Kama Rais alivyokuwa akitoa hotuba yake bungeni alisema ngombe wetu akichinjwa nyama yake haiwezi kuzidi kilo 150 hii yote ni kutoka na kutokuwa na utafiti wa mbegu bora ambazo zitaweza kutoa kiasi cha kutosha cha nyama”amesisitiza

Aidha amesema kuwa pia TALIRI inatakiwa kufanya tafiti ya mbegu bora za ngombe ili kuwa na uhakika wa nyama ya kutosha pamoja na maziwa.

“Lazima sekta hii ya mifugo tui ‘link’ na Tanzania ya viwanda hivyo basi tunatakiwa kuhakikisha kuwa ngoimbne wetu wanatoa nyama ya kutosha na iuliyobora,maziwa mengi,ngozi pamoja na pembe pamoja na kwato”amesema

Aidha amesema  kuwa kama sekta ya mifugo itashindwa kuwa na bidhaa zitokazo na mazao ya mifugo bora hata malighafi kwa ajili ya viwanda hazita kidhi viwango.

Ameongeza kuwa ni wakati sasa kwa Taasisi hiyo kukaa mguu sawa siraha begani ili kuzalisha mifugo bora na kukuza sekta ya mifugo.

Hata hivyo ameiagiza TALIRI kuhakikisha kuwa wabunifu katiika kuangalia chanamoto mpya zinazohusu wafugaji na nchgi ili kuzifanyia kazi mara moja.

Awali Mwenyekiti wa wa baraza hilo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TALIRI Dk. Jonas Kizima, amesema kuwa kiakao hicho ni cha pili kwa baraza hilo na moja ya kazi yake ni kupitia bajeti yake.

“Pamoja na kupitia bajeti pia mweshimiwa katibu mkuu tutakuwa na maazimio ambayo tutayaandika na kukuletea wewe ikiwa ni sehemu ya utekelezaji kwa ajili ya utekelezaji”amesema Kizima