Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mbunge wa Kikwajuni), akikabidhi vifaa vya michezo kwa washiriki wa Mashindano ya Masauni na Jazeerah Cup, katika Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mbunge wa Kikwajuni), akieleza kuhusu umuhimu wa umoja na mshikamano kupitia Mashindano ya Masauni na Jazeerah Cup, katika Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar, yanayoshirikisha timu 20 za mpira wa miguu katika jimbo hilo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mbunge wa Kikwajuni), (wa tatu kulia) akikabidhi mipira ya miguu kwa washiriki wa Mashindano ya Masauni na Jazeerah Cup, katika Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar, Mhe. Nassor Ali Jazeerah, akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo washiriki wa Mashindano ya Masauni na Jazeerah Cup, zilizotolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mbunge wa Kikwajuni) (hayupo pichani) na Mwakilishi huyo.
Mdau wa Michezo Bw. Salum Ali, akimshukuru Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mbunge wa Kikwajuni) (hayupo pichani), na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar, Mhe. Nassor Ali Jazeerah kwa kuthamini michezo ambayo imekuwa chachu ya umoja na mshikamo ndani na nje ya Jimbo hilo.
***********************************
Na. Peter Haule, WFM, Zanzibar
NAIBU Waziri wa Fedha na MIpango, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani za zaidi ya shilingi milioni 20 na kuzindua ligi ya Masauni & Jazeerah itakayoanza kutimua vumbi Alhamisi Juma hili katika viwanja vya Tumbaku, Miembeni-Zanzibar.
Masauni amesema kuwa ligi hiyo itakayozishirikisha timu 20 inalenga kuamsha ari ya michezo na kufufua kandanda visiwani humo hususan Jimbo la Kikwajuni ili kukuza vipaji vya vijana na ajira.
Mhandisi Masauni amesema kuwa Jimbo lake lilikuwa kinara wa mchezo wa soka miaka ya nyuma ikiwemo timu ya Small Simba ambayo ilitikisa katika medani za soka lakini cheche hizo zimezima ndio maana wakaanzisha michuano hiyo ya Masauni & Jazeerah iliyotimiza miaka 6 sasa tangu ianzishwe, ambapo imefanikisha kupatikana kwa vipaji vingi vya wachezaji na baadhi yao wanacheza ligi Kuu Zanzibar na Tanzania Bara.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nasor Ali Jazeera, alisema kuwa jitihada za kuendeleza soka zinakwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ya kutaka kukuza michezo.