***************************
WAGANGA Wafawidhi wa Zahanati na vituo vya Afya Katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamekutana leo kwenye kikao kazi kwa lengo la kuboresha huduma ya Bima ya CHF kwa wananchi ili waifahamu huduma hiyo.
Akizungumza katika kikao kazi hicho leo jijini Dodoma Mratibu wa CHF Mkoa wa Dodoma Dokta Francis Lutalala amesema kuwa wamekutana na waganga wafawidhi wa zahanati na vituo vya afya vyote vya halmashauri ya jiji la dodoma ambapo amesema kuwa waganga wahamasishe kila familia iwe na kadi ya mfuko wa bima ya afya CHF katika maeneo yao ili kuongeza mapato katika vituo vyao.
Aidha,Dkt Lutalala ametoa wito kwa waganga wazahanati na vituo vya Afya kuhakikisha wanatoa huduma bora na kuwa na luga nzuri kwa wateja na kuwashauri kuingia katika huduma ya Bima ya CHF ili kuimarisha huduma ya Afya kwa jamii.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa jiji la Dodoma Dokta Hendrew Method amesema kuwa wameweka mikakati chanya katika kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma bora katika maeneo yao huku mratibu wa CHF jiji la Dodoma Patrick Sebyiga amesema kuwa wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kila mwananchi anapata taarifa za CHF na waleo ambao hawajajiunga na huduma ya CHF wajiunge ili wapate hudma bora kwa garama nafu.
Naye Mganga mfawidhi zahanati ya zuzu Dokta Judica Sindato amebainisha kuwa ushirikiano wao na wananchi kwa ujumla wamefanikiwa kuwafikia wananchi wengi kwa kutoa elimu ya Bima ya AFYA na wengi kuifahamu na kujiunga kwenye bima hiyo.