


*****************************
NA NAMNYA KIVUYO, ARUSHA.
Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kimetoa mafunzo kwa maafisa ustawi wa jamii nchini ili kuweza kulinda na kutetea haki za makundi maalum wakiwemo wanawake, watoto na watu wenye ulemavu kutokana na kuendelea kupitia changamoto mbalimbali zinazopelekea kutokufurahia haki zao.
Akiongea wakati wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga alisema kuwa kituo hicho kina wa miaka mitani ambapo mpango namba nne umejikita katika kulinda na kutetea haki za makundi maalumu wakiwemo wanawake,watoto na watu wenye ulemavu.
” Makundi haya wameendelea kupitia changamoto mbalimbali duniani na nchini Tanzania hali iliyopelekea kutofurahia haki zao ambapo ripoti yetu ya Haki za Binadamu ya mwaka 2020 imeripoti kuwa kumekuwa na kesi zaidi ya elfu 26544 za ukatili kwa wanawake ikiwemo vifo 32 vya wanawake kuuawa na wenza wao,” Alisema Anna.
Alifafanua kuwa kanda zinazoongoza kea kwa ukatili huo ni Kanda ya ziwa,Kanda ya Magharibi na kanda ya mashariki ambapo pia ripoti imeripoti zaidi ya kesi 7263 za ubakaji kwa wanawake katika mikoa ya Dar es salaam,Kilimanjaro,Tanga,Mbeya na Dodoma.
Alieleza kwa mwaka 2019 ripiti hiyo imesema zaidi ya kesi elfu 4397 za ukatili wa kingono kwa watoto zimeripotiwa huku kukiwepo kwa ongezeko la ukatili wa kimwili,ndoa za utotoni pamoja na ukeketaji na mikoa inayoongoza kwa ukatili huo ni Shinyanga, Tabora, Mara, Lindi na Mirogoro.
Aidha alieleza kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali za utekelezaji na ulinzi wa watoto wanaokinzana na sheria,wanaoingiliana na sheria na wanaoathirika na ukatili ambao upatilanaji haki kwao umekuwa changamoto mara nyingi jammbo ambalo linaonyesha kuwa maagisa ustawi wa ni ni wadai muhimu katika usimamizi wa haki za watoto.
“Kwa kutambua umuhimu wa maafisa hawa kituo chetu kimeungana na TAMISEMI kuwajengea uwezo maafisa ustawi 150 hapa nchini ambapo lengo letu ni kueafikia maafisa ustawi 740 nchi nzima,”Alifafanua.
Kwa upande wake mkurugenzi huduma za ustawi wa jamii kutoka ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Rasheed Maftah alisema kuwa serikali ina sera na mikakati mbalimbali inayoitekeleza ili kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa miaka mitano ambao umeanza mwaka 2021 hadi 2022.
“Tunataka hadi kumalizika kwa mkakati huo tuwe tumetokomeza ukatili kwa watoto kwa asilimia 50 kwani pamoja na jitihada zote tunazozifanya bado kuna changamoto ikiwemo mimba za utotoni,”Alisema Maftah.
Alieleza wanatekeleza mkakati wa miaka mitani wa kutokomeza ulatili ambapo hadi hivi sasa wameshaanzisha kamati za ulinzi na usalama wa watoto na wanawake mikoa yote na katika halmashauri zote 184 pamoja na ngazi za kata vijiji na mitaa ambazo zimekuea niza msaada sana dhidi ya ukatili.
“Kamati hizi zinatisaidia kupata taarifa mapema na kuweza kuzuia ukatili uliotaka kujitokeza na kuchukia hatua lakini pia tunaendelea kuwaelimisha maafisa ustawi ili waweze kuwa na weledi mkubwa katika kufanya kazi,” Alieleza.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo FaithMery Lukindo kutoka Sengerema na Jahnson Lukindo kutoka Kilimanjaro walisema kuwa mafunzo hayo yatawapa uimara wa kusimamia kesi ili kuhakikisha makundi hayo yanapata haki zao.
Aidha walieleza sababu zinazopelekea ukatili kutokea ni pamoja na mila potofu, malezi ya kambo, pamoja na kukosekana kwa maadili katika jamii ambapo mafunzo hayo yatawawezeshavkuongeza juhudi za kupambana na ukatili katika maeneo yao ya kazi.