************************
.
Msanii wa Bongo Movie ambaye pia ni Mtangazaji wa radio EFM , Dkt.Kumbuka ameamua kushabikia klabu ya Simba na kuachana na klabu ya mwanzo ya Yanga.
Dkt.Kumbuka amesema kuwa uwamuzi huo aliochukua hajalazimishwa na mtu yoyote bali ni namna alivyoona klabu hiyo ya Simba ikifanya vizuri kwenye michuano mikubwa hivi karibuni.
“Ukiwa shabiki wa Simba unapata raha, nimekuwa chawa gegedu wa vunja bei na chawa gegedu wa klabu ya Simba kuanzia leo hii”. Amesema Dkt.Kumbuka.