*********************
Rais Mteule wa Chad, Idriss Deby amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa mapambano dhidi ya Waasi.
Jeshi la Chad limetangaza kuwa Rais Idriss Deby amefariki dunia baada ya kupata majeraha kwenye mapambano dhidi ya waasi.
Jeshi la Chad kwa sasa linapambana na waasi ambao walifanya mashambulizi wakijaribu kuuteka mji mkuu N’Djamena
Rais Deby amefariki dunia saa chache baada ya kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo kuwa mshindi wa kiti cha Urais.