**********************************
NJOMBE
Wakulima wa zao la chai pamoja na wawekezaji wa viwanda vya kuchakata majani ya chai nchini wameiomba serikali kuharakisha uanzishwaji wa mnada wa chai jijini Dar es salaamu ili kuokoa mitaji ya wawekezaji na wafanyabishara wa ndani ya nchi ambao wanatumia zaidi ya mil 6 kusafirisha kontena moja la majani kwenda nchini Kenya katika mnada wa Mombasa.
Wakizungumza katika mafunzo yaliotolewa na MAKEUP kwa ufadhiri wa umoja wa ulaya yaliokutanisha wakulima wawekezaji wa viwanda vya chai kutoka mikoa mitano nchini ukiwemo Njombe yenye lengo la kuwapa mbinu na kuwajengea uwezo wa kufanya biashara hiyo kwa tija wadau wa sekta ya chai wanasema wanatumia zaidi ya mil 6 kusafirisha kontena moja la maji kwenda Mombasa Kenya huku endapo mnada ungekuwepo nchi ingekuwa chini ya mil 3
Kufuatia hali hiyo Gerard Ngenzi ambaye ni meneja wa kiwanda cha Chai Ikanga na Kenedy Pita mkulima wa chai kutoka Tarime mkoani Mara wanasema serikali ione ulazima wa kuharakisha uanzishwaji wa mnada wa chai nchini ili kunusuru sekta ya chai na kisha kuokoa fedha zinazoenda kenya.
Akifafanua jitihada za serikali kuhusu kilio cha wakulima na wawekezaji wa viwanda vya chai Fikiri Katiko ambaye ni afisa Masoko wizara ya kilimo amesema serikali imeona changamoto hizo katika sekta ya chai hivyo wapo kwenye mchakato wa kuanzisha mnada ndani ya nchi pamoja maabara ya kupima majani ndani ya nchi jambo ambalo litaleta afya katika maendeleo ya sekta hiyo muhimu.
Akieleza sababu ya kuingia katika kilimo cha chai na matarajio ya mradi katika kuendeleza sekta ya chai maratibu wa mradi wa Makeup nchini Safari Fungo amesema ni kutokana na uhitaji wa bidhaa hiyo sokoni na kudai kwamba mradi unakwenda kuwaunganisha wafanyabishara na masoko ya umoja wa ulaya sambamba na kutoa usaidizi wa nyenzo.
Wadau kutoka mikoa takribani 5 ukiwemo wa Mara,Iringa,Mbeya,Tanga na Njombe wameshiriki katika mafunzo hayo.