********************************
Klabu ya Simba bado inaendelea kuonesha ubabe wao kwenye timu pinzani baada ya kuichapa Mwadui Fc bao 1-0 kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Dakika 45 Mwadui waliweza kuzuia mashambulizi ya Simba ambao walikuwa wakimtumia kiungo Rarry Bwalya na Clatous Chama kumtengenezea pasi Meddie Kagere na kufanya waende mapumziko ubao ukiwa Mwadui 0-0 Simba.
Dakika ya 66, Bocco alibaldili ubao ambapo ulisoma Mwadui 0-1 Simba na bao hilo lilidumu mpaka dakika ya 90 na kuwafanya Simba kusepa na pointi tatu kwa tabu mbele ya wapinzani wake leo.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 52 ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 22 imetofautiana pointi mbili na vinara Yanga wenye pointi 54 baada ya kucheza mechi 25.