…………………………………………………………………………….
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAFANYA UPELELEZI NA UFUATILIAJI MKALI KUFUATIA MATUKIO MAWILI YALIYO TOKEA KWA NYAKATI TOFAUTI KATIKA WILAYA YA NYAMAGANA.
TUKIO LA KWANZA,
TAREHE 16.04.2021 MAJIRA YA 08:00 HRS KATIKA MTAA WA IPULI, KATA YA MAHINA, WILAYA YA NYAMAGANA, ULIKUTWA MWILI WA MTU MMOJA ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA 35, AKIWA AMEUAWA NA KUTELEKEZWA ENEO LA MAKABURI. JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UPELELEZI WA KINA ILI KUBAINI WAHUSIKA NA KUWAKAMATA NA KUWAFIKISHA MAAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO KWA UCHUNGUZI ZAIDI.
TUKIO LA PILI,
TAREHE 16.04.2021 MAJIRA YA 06:00HRS HUKO MAENEO YA BUKAGA, KATA YA KISHIRI, WILAYA YA NYAMAGANA, VIJANA WAWILI JINSI YA KIUME AMBAO BADO KUFAHAMIKA UTAMBULISHO WAO, WANAOKADIRIWA KUWA NA MIAKA KATI YA 18-23, WALIUAWA KWA KUSHAMBULIWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO KWA KUPIGWA MAWE NA KUNDI LA WATU AMBAO BAADAE WALITAWANYIKA NA KUKIMBIA WALIWATUHUMU WATU HAO KUJIHUSISHA NA MATUKIO YA WIZI. ENEO LA TUKIO KULIKUTWA KUKU WATANO NA PIKIPIKI YENYE USAJILI MC 607 CPK MALI WALIZOTUHUMIWA KUIBA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO KWA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI. MSAKO MKALI UNAENDELEA MAENEO YOTE ILIKUKAMATA WALE WOTE WALIOHUSIKA NA MAUAJI HAYO KWA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWATAKA WAANCH KUACHA VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI KUFANYA HIVYO NIKUTENDA KOSA LA JINAI. NA WALE WOTE WALIOHUSIKA KWA MAUAJI HAYO WATAKAMATWA NA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
IMETOLEWA NA;
Muliro J. MULIRO- ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.