Home Mchanganyiko RC KUNENGE AMTAKA MKANDARASI ANAYEJENGA BARABARA YA MAKONGO KUKAMILISHA KABLA YA OCTOBER...

RC KUNENGE AMTAKA MKANDARASI ANAYEJENGA BARABARA YA MAKONGO KUKAMILISHA KABLA YA OCTOBER MWAKA HUU

0

………………………………………………………………………………..

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge leo April 17 amefanya ziara ya kukagua miradi minne ya maendeleo Jijini humo ambapo amemtaka mkandarasi kutoka kampuni ya JASCO Building and Civil Contractor anaejenga Barabara ya Makongo kuhakikisha inakamilika kabla ya Mwezi October.

RC Kunenge amezitaka Taasisi za DAWASA na TANESCO kufanya kazi kwa ushirikiano na Mkandarasi huyo kwa kuondoa miundombinu ya Maji na umeme iliyopita kwenye mradi ili mkandarasi asipate kisingizio chochote Cha kuchelewesha kazi.

Aidha RC Kunenge amesema Barabara hiyo yenye urefu wa Km 4.5 ni moja ya Barabara muhimu Katika kutatua changamoto ya foleni kwenye Barabara ya Bagamoyo ambapo Mradi huo umegharimu zaidi ya Bilioni 8.2.

Hata hivyo RC Kunenge ametembelea Ujenzi wa Barabara ya Madale kuelekea Wazo yenye urefu wa Km 6 inayogharimu Shilingi bilioni 9.7 ambapo amemuelekeza Mkandarasi kutoka kampuni ya MECCO kukabidhi Mradi mwezi wa tano mwishoni Kutokana na Barabara hiyo kuwa msaada mkubwa kwa Mabasi yaendayo Mikoa ya kaskazini yakitokea kituo kikuu Cha Mabasi Cha Magufuli.

Akiwa kwenye Ujenzi wa Daraja la Ulongoni A na B unaokwenda sambamba na ujenzi wa Barabara na kingo za mto, RC Kunenge ameonyesha kuridhishwa na utekelezaji wa Maagizo aliyowapa wakandarasi Jambo likilosaidia Ujenzi kufikia 70%.

Kutokana na hilo RC Kunenge ametaka Daraja la Ulongoni A kukamilika kabla ya Tar 10/06/2021 huku Daraja la Ulongoni B akitaka likamilike kabla ya Mwishoni mwa mwezi wa Sita.