………………………………………………………………………
Bahati Mollel, Mwanza
WENYEJI timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kesho wataumana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) katika mchezo wa soka utakaofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana jijini hapa.
Akitoa ratiba mara baada ya kikao na viongozi wa klabu zinazoshiriki kwenye michezo hiyo waliokutana jana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini hapa, Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Mei Mosi Taifa, Stanslaus Matimo amesema mechi nyingine ni kati ya Tanesco kucheza na Ukaguzi ya mchezo wa soka itakuwa kati ya.
Matimo amesema kwa upande wa mchezo wa netiboli kutakuwa na mechi tisa zote zitafayika kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni, ambazo ni timu ya Ulinzi itakayokutana na timu ya Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC); huku Ikulu watakutana na Uchukuzi; na Tanesco watapepetana na Wizara ya Mambo ya Nje.
Michezo mingine ya netiboli ni kati ya timu ya Mamlaka ya Majisafi na taka ya Mwanza (Mwauwasa) watakaocheza na Wizara ya Mambo ya Ndani; wakati timu ya Wizara ya Kilimo watakutana na Ulinzi; na Ikulu watakwaruzana na timu ya Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini TPDC).
Matimo amesema michezo ya kuvuta Kamba kwa wanaume na wanawake nazo zitaanza leo kuanza saa 5:00 asubuhi kwenye uwanja wa CCM Kirumba kwa timu ya Ukaguzi kuvutana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro; huku Mamlaka ya Majisafi na taka ya Mwanza (Mwauwasa) watakutana na Ulinzi ambapo mechi zote ni za wanaume; wakati kwa upande wa wanawake timu ya Taasisi ya Saratani Ocean Road watacheza Wizara ya Mambo ya Nje; na Wizara ya Kilimo watavutana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).
Amesema uzinduzi rasmi utafanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba tarehe 20 Aprili, 2021 na mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela; ambapo pia hatua ya makundi kwa upande wa mechi za soka na kamba zitakazoanza leo zitamalizika tarehe 24 April, 2021; wakati tarehe 24 April, 2021 kunakuwa na michezo ya baiskeli, karata na draft; huku tarehe 25 April, 2021 kutakuwa na michezo ya riadha na bao.
“Tunatarajia tarehe 28 Aprili, 2021 mechi za mshindi wa tatu katika soka na Kamba zitafanyika, na fainali itakuwa tarehe 29 Aprili, 2021.” Amesema Matimo.
Michezo hiyo inatarajia kushirikisha wachezaji zaidi ya 1000 kutoka kwenye Wizara na taasisi za umma.
Mwisho