Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akiongoza Mkutano wa Wadau wa Masuala ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM/EIA) uliofanyika Dar es Salaam.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geofrey Mwambe akichangia wakati wa Mkutano wa Wadau wa Masuala ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM/EIA) uliofanyika Dar es Salaam Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Bw.Exaudi Kigae akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa Masuala ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM/EIA) uliofanyika Dar es Salaam.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo (kulia) akiongea jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi wakati wa Mkutano wa Wadau wa Masuala ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM/EIA) uliofanyika Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt.Samuel Gwamaka akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa Masuala ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM/EIA) uliofanyika Dar es SalaamMwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Prof. Esnat Chaggu akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa Masuala ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM/EIA) uliofanyika Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba wakati wa Mkutano wa Wadau wa Masuala ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM/EIA) uliofanyika Dar es Salaam.Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa Masuala ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM/EIA) uliofanyika Dar es Salaam. Washiriki wakiwa katika Mkutano wa Wadau wa Masuala ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM/EIA) uliofanyika Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Mbatilo)
*********************
NA EMMANUEL MBATILO
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais Muungano na Mazingira Seleman Jaffo amewataka wawekezaji nchini kutumia nafasi walizonazo kutoa nafasi za ajira kwa watanzania na kuhakikisha wanashiriki vyema katika suala la ulipaji kodi ili nchi iweze kunufaika na sekta hiyo kikamilifu.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa wadau wa mazingira na wawekezaji mkoani dar es Salaam leo ambapo amewataka wawekezaji kuzingatia umuhimu wa utunzaji wa mazingira katika maeneo yao ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utunzaji wa mazingira.
Hata hivyo amewataka wawekezaji wote nchini kujiamini kwani serikali ipo bega kwa bega nao ili waweze kufanya kazi zao ipasavyo kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira kwani Hawapo tayari kuona shughuli za uwekezaji zinaathiri maisha ya watu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka amesema ili kuondokana na changamoto zinazojitokeza katika upatikanaji wa cheti kwa haraka wawekezaji wanatakiwa kufuata utaratibu uliopo ili kuweza kufanikisha.
“Mchakato wa tathimini ya Mazingira kuna wajibu wa muwekezaji anapaswa kuufanya ili andiko lake liweze kwenda haraka na cheti kiweze kutolewa kwa muda anatakiwa kuhakikisha ya kwamba anaumiliki halali wa ardhi husika na kwamba ameweka mahusiano mazuri na majirani”. Amesema Dkt.Gwamaka.
Aidha Dkt.Gwamaka amesema muwekezaji pia anatakiwa kugharamia utafiti wote wa eneo analomiliki na vilevile kuandaa andiko la tathimini ya athari kwa mazingira kwa maana kwamba anagharamia mpaka lile andiko.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Muhandisi Prof. Esnat Chagu amesema majadiliano yaliyofanyika katika siku hii anauhakika kwamba yamewajingea uelewa mwingi kwa wale wote ambao wameshiriki katika tukio hilo.
“Nina uhakika kabisa kwamba leo tumepata mawazo mazuri, tumepata elimu nzuri na elimu hiyo sio kwetu tu lakini ni elimu ya muhimu kwaajili ya Watanzania wote maana wote wapo kwaajili ya uwekezaji”. Amesema Prof.Esnat.