Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwao Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, Kijiji cha Muriaza, Wilayani Butiama, Mkoa wa Mara.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara (kushoto) akimpa pole Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, alipohudhuria mazishi ya Mama Mzazi wa Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi, Bi Monica Tongori, aliyezikwa katika Kijiji cha Muriaza, Wilayani Butiama, Mkoa wa Mara.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Chilo, mara baada ya mazishi ya Mama Mzazi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro yaliyofanyika nyumbani kwao Kijiji cha Muriaza, Wilayani Butiama, Mkoa wa Mara.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akitoa salam za rambirambi katika msiba wa Mama Mzazi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, Bi Monica Tongori, aliyezikwa katika Kijiji cha Muriaza, Wilayani Butiama, Mkoa wa Mara.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akitoa heshima za mwisho kwa Mama Mzazi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, Bi Monica Tongori, aliyezikwa katika Kijiji cha Muriaza, Wilayani Butiama, Mkoa wa Mara.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Majeshi Tanzania (JWTZ), Generali Venance Mabeyo, walipokutana katika mazishi ya Mama Mzazi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, Bi Monica Tongori, aliyezikwa katika Kijiji cha Muriaza, Wilayani Butiama, Mkoa wa Mara.