Afisa Tarafa wa tarafa ya Ererai Titho Cholobi akiongea na vikundi 42 vya wanawake,vijana na kwenye ulemavu vinavyotarajia kupokea mikopo.
Baadhi ya wanavikundi wakofuatili mafunzo wanayopewa kabla ya kupokea mkopo.
…………………………………………………………………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO,ARUSHA.
Jiji la Arusha limejipanga kuweka mpango mkakati wa kufuatilia fedha shilingi bilioni 3 ambazo zilikopeshwa kwa makundi ya wanawake, vijana na wenye ulemavu kutokakana fedha hizo kupita muda wa urejeshaji.
Akifungua mafunzo ya vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi, Afisa Tarafa wa tarafa ya Ererai Titho Cholobi aalisema kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya makundi hayo kuchukua fedha na kukaa bila kuzirejesha ambapo halmashauri hiyo inadai zaidi ya billioni 3.
Alisema kuwa fedha hizo ni za serikali na ni kodi za wananchi ambapo utoaji wake unania njema ya kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwapa fedha itayosaidia kukuza mitaji yao na baada ya kusaidika kuweza kuzirejesha lakini kuna wachache ambao wanachukua na kutokomea nazo sasa hawa tunataka wawe fundisho kea wengine.
“Tunaenda kuweka mpango ea kuzirejesha na hawa wataenda kuwa fundisho kwani wanatakiwa kurudisha fedha hizo ili ziweze kuwanufaisha wengine istoshe heakupewa kwa kujuana bali walikopeshwa warudishe,” Alisema Cholobi.
Aidha amevitaka vikundi 42 vilivyopata mafunzo kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanarejesha kwa wakati mkopo wa shilingi milioni 565.3 watakapatiwa na Halmashauri ya jiji la Arusha kwa uaminifu ikiwani pamoja na kutumia vyema mafunzo vizuri ili yaweze kuwasaidia katika utumiaji wa mikopo hiyo.
Cholobi alisema kuwa fedha hizo zinatokana na mapato ya ndani ya halmashauri na hazitolewi kwa watu kujuana bali kwa vikundi kufuata utaratibu uliopo ambapo amewataka vijana kujifunza kuaminika kwani fedha zinazotolewa ni fedha za walipa kodi ambazo zinapaswa kurejeshwa kwa wakati ili ziweze kukopeshwa watu wengine.
“Hii milioni 565.3 mtakayopewa kama mkopo baadhi ya halmashauri ndiyo mapato yao ya ndani hivyo mkatumie fedha hizo katika kusudi lililokusudia ili muweze kurejesha kwa uaminifu zaidi.”Alisema Cholobi
Kwa upande wake meakilishi wa mkurugenzi wa jiji hilo Mwanamsiu Dossi ambaye pia mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii jiji alisema kuwa halmashauri imeendelea kutenga fedha kutoka katika mapato ya ndani na kuelekezwa kwenye vikundi vya vijana,wanawake na wenye ulemavu .
Alifafanua kuwa fedha hizo zitakazotolewa ni fedha za miezi 6 za robo ya kwanza na robo ya pili ambapo zitabaki fedha za robo ya 3 na robo ya 4 katika utoaji wa mikopo na kusema kuwa mikopo hiyo inayotolewa inapaswa kurejeshwa na haitokani na fedha za ruzuku.
Naye Afisa vijana jiji la Arusha kwa niaba ya Afisa maendeleo ya jamii wa jiji hilo,Hanifa Ramadhani amesema kuwa kwa kipkndi cha mwezi Juni hadi Desemba halmashauri imeidhinisha utoaji wa mikopo yenye zaidi ya shilingi milioni 565 kwa vikundi 42 Bya wajasiriamali vilivyopo katika kata 23 za jiji la Arusha.
Aliongeza kuwa kati ya fedha hizo zaidi ya milioni 359 zitatolewa kwa vikundi 25 vya wanawake na zaidi ya shilingi milioni 175 zitatolewa kwa vikundi 15 vya huku fedha zaidi ya milioni 30 zitatolewa kwa vikundi 2 vya watu wenye walemavu amnapo amwsema vikundi hivyo ni vile vilivyopitishwa na kamati ya fedha na utawala.
Pamoja na hayo amesema kuwa halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa kadri itakavyokuwa ikipokea maombi kutoka kwenye vikundi na kulingana na fedha zitakazokuwa zikipatikana kutokana na makusanyo ya mapato ya ndani ya halmashauri na marejesho ya mikopo ya nyuma.
Mmoja wa wanavikundi hao aliyejitambulisha kwa jina la Neema Noel ameishukuru halmashauri hiyo kwa kuweza kuwapatia mkopo huo ambao amesema utamsaidia kuendeleza biashara yake.