Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya kumkabidhi Ofisi ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambayo pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali kwa Bw Gerson Msigwa iliyofanyika leo April 16,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambayo pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali kwa Bw Gerson Msigwa,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya Kukabidhiwa rasmi Ofisi yake Mpya iliyofanyika leo April 16,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambayo pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali kwa Bw Gerson Msigwa,akikabidhiwa rasmi nyaraka za kuendesha Ofisi na aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi,hafla hiyo imefanyika leo April 16,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambayo pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali kwa Bw Gerson Msigwa,akiangalia moja ya nyaraka mara baada ya kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi,hafla hiyo imefanyika leo April 16,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKURUGENZI wa Idara ya habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amesema kuwa atahakikisha anashirikiana na Waandishi wa habari kwa kuwapa taarifa zote wanazostahiki kuzipata ili ziwafikie Wananchi kwa wakati.
Msigwa ameyasema hayoleo April 16,2021 jiiini Dodoma hapa Wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Msemaji wa Serikali Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sànaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas.
Bw.Msigwa kuwa ili mambo yaendelee lazima wanahabari nchini wakubali kuilinda Serikali na kuutanguliza uzalendo kwa kufuata Sheria ,kanuni na taratibu za nchi.
” Nipo tayari kufanya kazi nanyi Wakati wowote,lakini lazima niseme ukweli kuwa nitakuwa mtu wa ajabu na nitasikitika Sana Kama ikitokea kwenye uongozi wangu kuona waandishi wa habari mnaharibu nchi kwa kwenda kinyume na utaratibu,”amesema Msigwa
“Nawaahidi kuwa mtapata taarifa mnazostahili kuzipata kutoka serikalini,hata hivyo lazima niwe mkweli sio kila kitu mtaambiwa,mtaambiwa vile tu mnavyostahili,”amesisitiza
Licha ya hayo amesema,Idara hiyo ya Habari-Maelezo ina Sheria ,taratibu na miongozo hivyo kuwahimiza wanahabari wote kuzingatia na kutokuwa wabinafsi wa kutanguliza maslahi yao mbele kuliko uzalendo.
“Waandishi wa habari niwaambie Kwenye kutimiza wajibu timizeni lakini kwa kufuata Sheria na kanuni za nchi ikiwa Ni Pamoja na kufuata misingi ya huduma za uandishi wa habari,”ameeleza
Hata hivyo amemshukuru Hayati Dkt.John Magufuli kwa kumpa dhamana ya Kazi kwa miaka mitano huku akisema kazi aliyoiacha Magufuli inaendelea kwa Mama Samia na kwamba kila kitu kitaendelea Kuwa sawa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ya habari Dkt.Abbas alimshukuru Rais Mhe.Samia kwa kuendelea kumwamini na kumpa nafasi ya kutumika Katika Serikali yake huku akisema kwa kipindi chote cha miaka minne na miezi nane ambacho amekuwa Katika nafsi ya msemaji wa Serikali amefarijika kuona Tanzania mpya ikiendelea kusimama.
Aidha Dkt.Abbas alimpa Wosia Msigwa kuwa makini na kazi hiyo “kazi ya msemaji wa Serikali ni Kazi Kama ya mwanahabari wa kawaida Inabidi usilale ikibidi kulala kimkakati,”amesisitiza