…………………………………………………………………………………….
Happy Lazaro, Arusha
Naibu katibu mkuu wizara ya katiba na Sheria Amon Mpanju amekitaka chama cha mawakili Tanganyika (TLS) kujikita kwenye misingi bora ya kuendeleza sheria na kuendeleza maadili ya taaluma ya tasnia hiyo huku wakitenda haki sawa kwa wananchi wanaohitaji huduma.
Mpanju ameyasema hayo leo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa chama Cha mawakili Tanganyika,(TLS) uliyofanyika jijiini Arusha .
Amesema kuwa,matarajio ya serikali ni kuona chama hicho kinatekeleza majukumu yake kitaaluma na kuwepo kwa maana halisi ya kuanzishwa kwake katika kuweka mazingira wezeshi kwa wanachama kuweza kunufaika na kuendeleza hiyo taaluma sambamba na kushughulikia mazingira na maslahi ya wanachama.
Aidha aliwataka kuhakikisha wanafuata maadili na sheria za kazi yao katika kuhudumia wananchi kwa kutenda haki kama ilivyo taratibu za sheria na kanuni.
Aidha Mpanju amewataka viongozi wapya wa chama hicho watakaochaguliwa kujitafakari na kuja na mikakati mipya ambayo itawezesha chama hicho kuendelea kuwa imara na kuleta manufaa kwa wanachama wake huku wakiwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wananchi.
Hate hivyo aliwataka mawakili kuzingatia sheria na taratibu zilizopo katika kufanya kazi zao na kudumisha ulinzi na usalama huku akiwataka kuchagua viongozi wenye matwaka ya kuhakikisha chama kinakuwa na tija .
Awali Rais wa chama cha mawakili Tanganyika ,Dokta Rugemezela Nshala akisoma risala yake kwa mgeni rasmi amesema kuwa wamekuwa wakikutana kila mwaka katika kuhakikisha wanajadili changamoto mbalimbali na kuweza kuzipatia ufumbuzi ikiwa ni njia mojawapo ya kukiboresha Cham hicho.
Amesema kuwa,viongozi wapya watakaochaguliwa ni vizuri wakajikita zaidi katika kutetea maslahi ya chama na wananchi wake kwa ujumla.
Mmoja wa wagombea pekee mwanamke katika nafasi ya urais Tls,Flaviana Charles amesema kuwa, anaona kuwa mchakato unaenda vizuri kwa ujumla japo Kuna ushindani mkubwa lakini anaamini kuwa atashinda.
‘mimi ni mwenyeji na siji kujifunza na nakuja na uzoefu ambao utapeleka chama katika hatua nyingine na amegombea kwa sababu anakijua Chama hicho na wanasheria wake sambamba na kujua changamoto ambazo chama hicho kinapitia hivyo wakinichagua Mimi hawatajutia kamwe”amesema.
Amesema kuwa, atawasaidia wanasheria wachanga wale ambao wameingia kwenye fani chini ya miaka mitano kwani wengi wao hawajui waanzie wapi na watajengewa uwezo namna ya kufanya kazi na kuona fursa mbalimbali zilizopo.
Amefafanua kuwa, atahakikisha anawasaidia katika uboreshaji wa ada na kuangalia namna ya kupunguza ada ambapo imekuwa ni kilio cha wanasheria wengi hasa wachanga kwa kutafuta njia mbadala ya kujipatia fedha kwa kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato.
Flaviana ameongeza kuwa, wanahitaji kufanya kazi na serikali katika kuhakikisha wanaboresha mahusiano na jamii pamoja na mahakama ,ambapo wanahitaji kuiwakilisha jamii kwa umakini na weledi mkubwa,sambamba na kuzifanyia kazi sheria mbalimbali zinazowakandamiza wananchi kwa kuzifanyia maboresho zaidi.