Home Michezo MAN CITY YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA, SASA USO KWA USO...

MAN CITY YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA, SASA USO KWA USO NA PSG

0

TIMU ya Manchester City ya England imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Borussia Dortmund usiku wa jana Uwanja wa Signal-Iduna-Park Jijini Dortmund, Ujerumani.
Jude Bellingham alianza kuifungia Borussia Dortmund dakika ya 15, kabla ya Man City kutoka nyuma kwa mabao ya Riyad Mahrez dakika ya 55 kwa penalti na Philip Foden dakika ya 75.
Manchester City wanakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-2 baada ya kushinda 2-1 pia kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Etihad na watakutana na PSG ya Ufaransa iliyowatoa waliokuwa mabingwa watetezi, Bayern Munich.