KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Dkt.Laurean Ndumbaro,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo April 14,2021 jijini Dodoma wakati akijibu tuhuma za aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof.Mussa Assad kuhusu tuhuma alizotoa hivi karibuni Kuwa asilimia 60 ya watumishi wa Umma hawafai na asilimia 40 wanao uwezo kidogo hivyo wale wasiofaaa wapigwe chini.
………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Dkt.Laurean Ndumbaro amewataka Watanzania kupuuza maneno ya aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof.Mussa Assad kuhusu tuhuma alizotoa hivi karibuni Kuwa asilimia 60 ya watumishi wa Umma hawafai na asilimia 40 wanao uwezo kidogo hivyo wale wasiofaaa wapigwe chini.
Kauli hiyo ameitoa leo April 14,2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habaro amesema kuwa kauli iliyotolewa na Mstaafu huyo Wakati akihojiwa na waandishi inatia ukakasi kwa watumishi wa Umma na haina ukweli wowote .
Dkt.Ndumbaro amesema kuwa Ofisi hiyo Kama msimamizi wa masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala bora ametoa wito kwa jamii kutambua Kuwa Utumishi wa Umma unajengwa na kuongozwa na misingi ya katiba , Sheria ,taratibu , kanuni na miongozo mabalimbali ambapo nyaraka hizo ndizo zinaongoza na kuelezea vigezo na sifa za ajira na ngazi za vyeo vya uongozi.
“Sisi tukiwa Wenye dhamana ya masuala ya Utawala bora tumeona tutoe ufafanuzi wa Jambo hii kwamba halina ukweli wowote na jamii haipaswi kusikiliza vitu ambavyo vinatolewa na mhemko na hisia binafsi bila kufanya uchunguzi,”amesema Dkt.Ndumbaro
Aidha amesema Kuwa watumishi wa Umma wanaelewa taratibu za Utumishi Kuwa mtumishi anayepaswa Kuwa kiongozi lazima awe amefikia ngazi ya uandamizi Katika kada yake.
” Nyaraka hizi Pamoja na Mambo mengine zinasaidia kujenga usawa katika ajira na uongozi,utu,heshima ya watanzania hadhi ya viongozi ,miiko na maadili Katika uongozi na Utumishi wa Umma,”amesisitiza
Kama kweli ni asilimia 60 ya watumishi hawafai na 40 wanafaa yeye yupo kundi gani?!alihoji”
Pamoja na hayo Dkt.Ndumbaro alisema viongozi na watumishi wa Umma huajiriwa na kuteuliwa kwa kufuata misingi hiyo hata zoezi la vyeti feki lilidhihirisha wazi kwa Kuwa ni asilimia 2.8 tu ya watumishi ndio waligundulika hawana sifa za Kuwa watumishi wa Umma.
“Nafikiri kabisa Prof.Assad aliongozwa zaidi na hisia kuliko uwezo wa akili na kitaaluma ambao anao,sisi Katika taaluma tunaamini kabisa bila utafiti huna uwezo wa kuzungumza,hivyo Mstaafu huyo hakuzingatia vigezo hivi,”amesema na kuongeza;
“Nasema hivyo kwa maana kubwa mbili,yeye vigezo alivyotumia vya kuwatuhumu viongozi wa Umma kwamba hawafai au wanafaa amedai Kuwa wamekuwa ni waoga na kutojiamini kwa watumishi,nimwambie tu Katika Utumishi wa umma suala la Kutoa ushauri katika ngazi mbalimbali unatolewa kwa wazi au Siri na Siri kuu kuendana na ngazi ya kitu husika hivyo asingeweza kufanya hivyo alipaswa Kutoa ushauri kwa kufuata taratibu,”amesisitiza.