******************************
NA NAMNYA KIVUYO,ARUSHA.
Imeelezwa kuwa uboreshaji wa miundombinu ya shule utaongeza uafanisi katika kukuza taaluma kutokana na mazingira ya kujifunzia na kufundishia kuwa rafiki.
Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Kennan Kihongosi eakati akiweka jiwe ya msingi katika majengo manne ya shule tatu za sekondari zilizopo ndani ya jiji la Arusha ambazo ni Moivo, Mkonoo pamoja na Kinana.
Kenan serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi ya uboreshaji wa miundombinu ya shule ili kuhakikisha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa walimu na wanafunzi yanakuwa rafiki na kuweza kutoa na kupata elimu bora.
“Kwa jiji la Arusha peke yake imegharimu zaidi ya milioni 900 ambapo tunaamini majengo haya yataongeza ufanisi na kupandisha kiwango cha taaluma katika shule hizi lakini nampongeza Rais wetu mheshimiwa Samia Suluhu kwa kuendeleza kazi ambayo hayati Rais Magufuli aliicha,” Alisema Kenan.
Alisema kuwa baada ya kuona ubora wa majengo hayo ni imani yake kuwa fedha zilizotolewa na halmashauri kwaajili ya miradi hiyo imetumika vizuri lakini pia aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili kesho na kesho kutwa waitumikie nchi yao kwa kuwa viongozi wa Tanzania ambapo aliwasihi watakapopata nafasi hizo kuwa wazalendo wa keli kwa kuweka maslahi ya nchi mbele.
“Taifa linawekeza kwenu nyie vijana wadogo kwasababu nyie ndio Tanzania ya baadae, tunaimani sana na nyie jitahididi kusoma na baadae mje kuweka na kuendeleza heshma ya nchi yenu, uzalendo uje kuwa dira yenu ya kuwaongoza,”Alieleza
Aliwaeleza kuwa pia wana wajibu wa kutunza miundombinu ya shule lakini wawaheshimu walimu wao pamoja kujiheshimu wenyewe nidhamu iwe kipambele chao.
Kwa upande wake naibu meya wa jiji la Arusha Veronika Hosea aliwataka wanafunzi kuhakikisha mafanikio yao kitaaluma yanaendana na majengo mazuri waliyojengewa na serikali.
Naye diwani wa kata ya Moivaro Philemon Meijo Mollel alisema pamoja na ujenzi wa madarasa na jengo la utawala bado kuna changamoto ya upatikanaji wa maji ambapo ameiomba serika kuwatengenezea magata na kuwekea mateki kwaajili ya kuvuna maji ya mvua na kuwayatumia kwa wakati huu ambao wanaendelewa kuisubiri mamlaka ya maji na usafi wa mazingira(AUWSA) wawafikisie huduma ya maji.
“Yakiwekwa magata hapa na mateki yakapatikana itasaidia upatikanaji wa maji hapa na itasaidia watoto hawa wasiende kuchota maji kwenye makorongo,”Alisema Diwani Meijo.
Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Moivaro Jackline Laizer aliishukiri serikali kwa kuwaboreshea miundombinu ya shule yao kwani awali walikuwa wanasoma kwa kubanana lakini tatizo lililobaki ni changamoto ya maji ambayo wanaenda kuchota kwenye makorongo hali inayopelekea kuchelewa kuingia darasani.
Afisa elimu sekondari wa halmashauri wa jiji la Arusha mwalimu Valentini Makuka
alisema kuwa bajeti ilikusudia kujenga madarasa 16 ambayo ndio upongufu uliokuwepo na majengo ya utawala 5 ambapo hadi sasa wamevuka lengo kwa upande wa madarasa kwa kuweza kupata madarasa 23 ambayo baadhi yalikuwa kama ofisi za walimu.
Mwalimu Makuka alieleza kuwa wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza walikuwa elfu 11,700 na walioripoti hadi sasa ni wanafunzi elfu 9800 na waliobaki wameenda shule binafsi.
“Kila mwaka asilimia 15 ya wanafunzi wanaofaulu hawaripoti kutokana na kwenda shule binafsi na tumefanya sensa hawa zaidi ya 1000 kila mmoja tunajua shule aliyopelekwa.