************************************
14,April
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
KATI ya watoto 100 wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Pwani,watoto 24 wana Udumavu na hii imetokana hasa na familia zao kuwa duni hivyo kushindwa kuinua uchumi wa familia hizo.
Pamoja na hilo, hali ya usajili katika mfuko wa Bima ya afya ya jamii (CHF)hairidhishi ,hadi sasa ni kaya 10,038 pekee sawa na asilimia 5.1 zimejiunga na mfuko huo kati ya kaya 294,634 .
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,aliyaeleza hayo katika kikao cha tathmini ya tatu ya utekelezaji wa mkataba wa lishe mkoani hapo.
Alieleza ,hali ya udumavu kwa mkoa ni 23.8 ukilinganisha na ule wa Taifa 30.1.
Hata hivyo alifafanua kwamba ,tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa kipindi cha Julai hadi Disemba 2020 ulivyotekelezwa ngazi ya halmashauri ni halmashauri sita ndizo zilizofanya vizuri.
“Utoaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za lishe ni sh.1,000 kwa kila mtoto kwa mwaka na halmashauri sita zimetoa zaidi ya asilimia 90.
Ndikilo alielezea, halmashauri tatu ikiwemo Mafia hali hairidhishi na ina asilimia 28.8 tu,Kibaha Mji 79.1 na Kibiti asimilia 58.5.
Hata hivyo ,mkuu huyo wa mkoa,alieleza hali duni husababisha kinga ya mwili kuwa duni na kudumaa ,hivyo mwili hushindwa kupambana na vimelea vya magonjwa mbalimbali ,Ili kupunguza gharama kubwa za matibabu ni muhimu kila kaya kujiunga na mfuko wa Bima ya afya ya jamii (CHF).
Mkuu wa wilaya ya Kibiti GulamHussein Kifu alisema ukiwepo,upungufu wa dawa kwenye vituo vya huduma ya afya inachangia kuwepo na muitikio mdogo kwa wanaojiunga na ICHF.
Nae Mganga mkuu wa mkoa wa Pwani ,dkt.Gunini Kamba alibainisha, uhaba wa dawa sio wa kutisha hivyo unafanyika utaratibu wa kuhakikisha dawa zinapatikana kwa wingi kwenye zahanati na maduka ya dawa yaliyopo kwenye hospitali..