*************************
NA VICTOR MASANGU, PWANI
SERIKALI mkoani Pwani imepanga kuendesha zoezi la ugawaji wa vitambulisho vipatavyo elfu 61 000 kwa kwa wafanya biashara wadogo wadogo pamoja na watoa huduma wadogo kwa kipindi cha mwaka 2021 ambavyo vitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa wa kuweza kuwapa fursa wafanyabiashara hao kuendesha shughuli zao za kujipatia kipato bila kusumbuliwa.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo wakati wa kikao maalumu ambacho kiliandaliw kwa lengo la kujadili utoaji wa Vitambulisho vya wafanyabiashara na watoa huduma wacogo kilichofanyika mjini Kibaha na kuwahusisha wakuu wawilaya, wakurugenzi, maofisa biashara , na viongozi wa wafanyabiashara wa Mkoa huo.
Aidha Ndikilo katika kulifanikisha zoezi hilo la kutimiza malengo waliyyojiwekea ametoa maelekezo kwa Halmashauri zote tisa za Mkoa huo kuhakikisha wanaweka nguvu kwenye utoaji wa Vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogowadogo.
Ndikilo alisema kuwa kuwepo kwa utaratibu huo kutaweza kuleta mabadilikomchanya kwa wafanyabiashara hao pamoja na kuweza kufanikiwa endapo pia vitaundwa vikosi kazi vitakavyofanyakazi kuanzia ngazi ya kitongoji na mitaa na kwamba nia ya serikali ni kuwasaidia wafanyabiashara hao.
“Kikao hiki tunajadili mambo mbali mbali na kwamba kwa kipindi hiki tunatarajia kugawa Vitambulisho 61,000 ambavyo vitaleta makusanyo ya zaidi ya sh. Bilion 1.2 vilivyotolewa kwa mwaka huu ni lazima kukaa na viongozi viongozi kuanzia ngazi ya Kijiji ili kupeana malengo kwa kila ngazi kuhamasisha wafanyabiashara waliopo kwenye maeneo yao kutumia fursa hiyo vizuri,”alisema Ndikilo.
“Tunatakiwa pia kuweka utaratibu wa kuwafikia wafanyabiashara wadogowadogo na watoa huduma kwenyw maeneo yao badala ya kuwasubiri kufika kujisajili kwenye ofisi” alisisitiza Ndikilo.
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Dr Delphine Magere alisema kwamba lengo la Serikali ni kuhakikisha inaweka mpango madhubuti ambayo itawasaidia wafanyabiashara wadogowadogo kupata Vitambulisho hivyo.
Naye Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogowadogo Wilaya ya Kibaha Philemon Maliga alisema kwasasa bado elimu haijatolewa kwa wafanyabiashara walengwa ambao ndio wanufaika wa Vitambulisho hivyo.
Alisema wafanyabiashara endapo Elimu itawafifika kama inavyotakiwa watachukua kwa wingi kwani Vitambulisho chasasa kimefanyiwa maboresho.
“Tumeshafikisha maombi Serikalini ulishaanza ombi Serikalini maofisa biashara wafike kwa wafanyabiashara kutoa Elimu kuhusiana na Vitambulisho vipya” alisema.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Geoffrey Kamugisha alisema wataalamu wanatakiwa kusaidia katika mfumo unaotumiwa kwenye malipo ya Vitambulisho hivyo lakini pia kuweka lugha rafiki kwa walengwa