Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya akimuelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange, alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa Vihenge vya kisasa, maghala pamoja na majengo ya ofisi, ujenzi uliofanywa mkoani Manyara na Kampuni ya Unia Sp.o.o ya nchini Polland, kwa gharama ya shilingi bilioni 18.59 na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Mhandisi Mkazi wa mradi wa Ujenzi wa Vihenge vya kisasa katika kituo cha Babati mkoani Manyara Baraka Mpembeule, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (katikati), alipokuwa akikagua mradi huo.Muonekano wa sehemu ya mizani, ofisi na maabara katika eneo la mradi wa ujenzi wa vihenge vya kisasa, ujenzi uliofanywa mkoani Manyara na Kampuni ya Unia Sp.o.o ya nchini Polland, kwa gharama ya dola za Kimarekani milioni 8.08 na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Vihenge hivyo vina uwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 40,000 za mazao.
Muonekano wa vihenge vya kisasa katika kituo cha Babati mkoani Manyara, vilivyojengwa na kampuni ya Unia Sp.o.o ya nchini Polland, kwa gharama ya shilingi bilioni 18.59 na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Vihenge hivyo vina uwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 40,000 za mazao.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.