Takribani wiki mbili baada ya itel kumtangaza balozi wake ambaye ni Diamond platnumz, sasa imebainishwa sababu za Diamond platnumz kuipenda simu hiyo ambayo ni tolea jipya la itel A37 ambayo imezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa sababu zilizoelezwa na Diamond kuhusu itel A37 ni pamoja na ubora na ukubwa wa skrini ya A37 ambayo ina 5.7” HD+ Waterdrop ikiwa ni full skrini.
Kabla ya uzinduzi huo Diamond aliwaambia wafanyabiashara ambao ni wadau wa
“itel A37 ni lazima niwe nayo kila siku ina skirini kubwa inatoa mwonekano bomba wa chochote ninachokitazama kwenye skrini ndio sababu naipenda sana na kizuri zaidi simu hii ina face unlock” amenukuliwa Diamond.
Kulingana na maelezo ya kampuni ya itel, face unlock ni mbadala wa fingerprint na hufanya kazi kwa ufanisi na ni salama na rahisi, ili kufungua itel A37 mtumiaji atatakiwa kutazama kwenye skrini ya A37 na simu itajifungua yenyewe.
Mbali na hilo itel A37 imeundwa kwa namna ambayo kama mtumiaji anataka kujipiga picha maarufu sefie na asingependa kubofya kwa kidole basi anaweza kutabasamu tu mbele ya kamera ya itel A37 na hapo atakuwa tayari ameshajipiga picha.
Kikubwa zaidi itel A37 imedizainiwa ikiwa na ukanda maalum mzuri wa kuvutia (ribbon), hii inakumweka mtumiaji kwenye ulimwengu wa fasheni mahali popote anapokuwepo.
Zaidi ya hayo, simu ya itel A37 imewekewa ulinzi wa macho kwa mtumiaji, hii inajulikana kama eye care ambapo mtumiaji atatumia simu hiyo kusoma vitabu ama kutazama chochote kwa mwanga laini usio na mionzi inayoumiza macho.
Simu hiyo iliyozinduliwa ina rangi tatu ambazo ni, Dark Blue, Light Purple, Gradient Green.
Rangi za itel A37 Dark Blue, Light Purple, Gradient Green