Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine Cha kilimo SUA Prof. Maulid Mwatawala (Wa kwanza kulia) akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo yatakayofanyika Chuoni hapo mwezi huu mwishoni kulia kwake ni Prof. Samweli Kaboto Mwenyekiti wa kamati ya mandalizi ya madhimisho hayo..
Mwenyekiti wa kamati ya maadhimisho hayo Prof. Samweli Kabote ( Wa kwanza kushoto) akitoa akizungumzia maandalizi hayo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuongea na waandishi wa habari Katikati ni Prof. Maulid Mwatawala kaimu Makamu Mkuu wa Chuo na Bi. Mariam Mwayela (wa kwanza kulia) Afisa mahusiano na masoko wa SUA.
Afisa Mahusiano na Masoko wa SUA Bi. Mariam Mwayela (wa kwanza kulia) Akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkuatano huo wa Waandishi wa habari,
Washiriki wa mkutano huo na Wandishi wa habari wakifuatilia taarifa inayotolewa kuhusu Maadhimisho hayo ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi Ujao,
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimeahidi kunedelea kuenzi mchango wa Aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu Hayati Edward Moringe Sokoine kutokana na ushupavu wake kama kiongozi katika kusimamia uchapa kazi,Kilimo vijijini,Uzalendo na kuchukia rushwa.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo ambeye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Upande wa taaluma Prof. Maulid Mwatawala kwa wakati akiongea na Waandishi wa habari Chuoni hapo juu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine kwa mwaka 2021.
“Chuo kiliamua kutekeleza maamuzi ya kuadhimisha siku hii kuanzia mwaka 1992 kwakuwa kiongozi huyu alikuwa mchapakazi na alipigania ,masuala ya kilimo hasa katika mapinduzi vijijini na utoshelevu wa chakula kwa watanzania” Alisisitiza Prof. Mwatawala.
Prof. Mwatawala ameongeza kuwa katika kipindi cha uongozi wake Hayati Sokoine alipiga vita suala la rushwa na kuimarisha uadilifu katika utumishi wa umma ambapo serikali iliyopo madarakani inayazingatia na kuyaenzi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Kaimu Makamu huyo wa Mkuu wa Chuo alibainisha kuwa Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yatafanyika kuanzia tarehe 24-27 Mei, 2021 Chuoni hapo baada ya kuhairishwa hapo awali kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt.John Pombe Magufuli.
Aidha alisema Mambo yatakayofanyika katika wiki hiyo Maonesho ya Teknolojia na ubunifu katika Kilimo, Ufugaji na Uvuvi, kufanya Mkutano wa kisayansi kwa Wanataaluma, Watafiti, Wanafunzi na wadau mbalimbalii, Mdahalo wa kitaifa wa Kumbukizi ya Sokoine utakaofanyika siku ya tarehe 27 Mei 2021,kutoa huduma za afya kwa binadamu hususani magonjwa yasiyoambukiza,Kutoa huduma za tiba ya mifugo kupitia hospitali ya rufaa ya wanyama bure kwa jamii, kuchangia damu salama na Kufanya michezo mbalimbali ambayo itaambatana na zawadi kwa washindi.
.
Hayati Edward Moringe Sokoine alifariki dunia kwa ajali ya gari Aprili 12, 1984 akiwa na umri wa miaka 46 katika Mkoa wa Morogoro akitokea Dodoma katika kikao cha Bunge na katika kipindi chake cha uongozi alihudumu kwa vipindi viwili.
“Kwa mwaka huu 2021 itakuwa ni maadhimisho ya 17 kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine toka kumbukizi ya kwanza mnamo mwaka 1992 ya maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka Chuoni ” alisema prof. Mwatawala
Awali akimkaribisha mgeni rasmi mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kumbukizi ya hayati Edward Sokoine Moringe Prof. Samweli Kabote kutoka SUA amesema kuwa Huwezi kuongea historia ya Chuo cha Sokoine cha Kilimo SUA bila kumtaja hayati Edward Moringe Sokoine kwa sababu Chuo kimebeba jina lake.
Wiki ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo, Teknolojia za kilimo, kuzalisha kwa tija na ushindani katika Soko, Kuelekea Nchi ya Uchumi wa juu wa Kati.