TIMU ya Liverpool leo imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Aston Villa Uwanja wa Anfield katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Ollie Watkins alianza kuifungia Aston Villa dakika ya 43, kabla ya Mohamed Salah kuisawazishia Liverpool dakika ya 57 na Trent Alexander-Arnold kufunga la ushindi dakika ya 90 na ushei.
Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 52 na kupanda nafasi ya tano, ikizidiwa pointi mbili na Chelsea baada ya wote kucheza mechi 31.