Mbunge wa Jimbo la Kalenga Jackson Kiswaga akimkabidhi mkuu wa Shule ya sekondari Lipuli,Peter Mbata saruji na vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya shule hiyo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa,Bashir Muhoja kulia akizungumza na mbunge wa Jimbo la Kalenga Jackson Kiswaga
…………………………………………………………………………………….
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MBUNGE wa Jimbo la Kalenga mkoani Iringa , Jackson Kiswaga amechangia,
shillingi millioni 46 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya mfuko wa jimbo lengo la ujenzi wa miundo mbinu ya shule na ujenzi wa madarasa na mabweni katika kata zote za Jimbo hilo.
Akizungumza kwenye ofisi ya mkuu wa shule ya sekondari Lipuli , Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Vijijini Bashir Muhoja alisema kuwa mbunge huyo ametoa fedha hizo za mfuko wa jimbo ambazo zimepelekea kuunda bodi ambayo hadi sasa imekuwa ikiendelea na uboreshaji wa miundombinu mashuleni.
Alisema kuwa mfuko wa jimbo na ni kitu ambacho kimeanzishwa na bunge na fedha hizi zinavyokuja zinakuwa na kamati yake
ndani ya halmashauri na imepokea fedha za majimbo yote mawili Jimbo la Ismani na Kalenga na baada ya kupitia vipaumbele na mahitaji ya husika.
Muhoja alisema kuwa Mbunge Kiswaga alitazama mahitaji yanayotakiwa kurekebishwa mapema kwanza ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Tanangozi na shule nyingine ndipo walipoelekeza fedha hizo zitumike.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kalenga, Jackson Kiswaga alisema kuwa nia ya serikali ni kuhakikisha inatatua changamoto zilizopo kwenye jamii na kutokana na fedha walizozipata ikapelekea kuunda kamati ambayo ilikuwa msaada kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu na madarasa mashuleni.
Alisema kuwa wanaishukuru serikali ya mama Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo anaendelea na kufanya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kwa kuendelea kufikia lengo lililokusudiwa
“Katika fedha ambazo huwa tunapatiwa mbunge huwa anaunda kamati na tukaangalia vipaumbele kulingana na mahitaji tuliyonayo kwa hiyo vipaumbele vyetu tulivyonavyo hasa kupunguza changamoto tuliyonayo kwa upande wa madawati lakini pia kuna ujenzi mwingine ambao unaendelea katika shule zetu pamoja na zahanati
.Kiswaga alisema kuwa wananchi wawe na imani naye kwani bado yupo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo itasaidia kuleta maendeleo katika jimbo hilo.
Naye diwani wa kata ya Kalenga, Shakira Kiwanga alisema kuwa anashukuru kwa utekelezaji unaoendelea pamojana kuahidi ujenzi kuanza mara moja kwani vitendea kazi tayari vimeshatengwa
Alisema kuwa viongozi watoe ushirikiano kwa kuwahamasisha wananchi kushiriki katika maendeleo pamoja na kutambua kazi inayofanywa na mh.mbunge kwani kwa kipindi cha nyuma katika shule ya sekondari Isakalilo wanafunzi walikuwa wanaingia kwa awamu ambapo changamoto hiyo imetatuliwa kutokana na fedha kiasi Cha sh milioni .12 kusaidia kuboresha eneo hilo hasa kwenye madarasa.
Mbunge Jackson Kiswaga amafanya utekelezaji huo kwa kutoa madawati 325 ambapo kwa shule ya lipuli ametoa madawati 20 pamoja na saruji itakayosaidia katika uboreshaji wa madarasa.