Kamishina wa Ushirikishwaji wa Jamii, Dkt Mussa Ali Mussa akikagua gwaride lililoandaliwa kwaajili yake katika viwanja vya gwaride vilivyopo katika kikosi cha kutuliza ghasia Morogoro tarehe 07.04.2020 alipokua katika ziara ya kukagua uwepo wa askari Kata na kukagua utekelezaji wa dhana ya Ushirikishwaji wa Jamii.
Kamishina wa Ushirikishwaji wa Jamii, Dkt Mussa Ali Mussa akipokea saluti kutoka kwa kamanda wa gwaride lililoandaliwa kwaajili yake katika viwanja vya kikosi cha kutuliza ghasia Morogoro tarehe 07.04.2020 alipokua katika ziara ya kukagua uwepo wa askari Kata na kukagua utekelezaji wa dhana ya Ushirikishwaji wa Jamii.
Kamishina wa Ushirikishwaji wa Jamii, Dkt Mussa Ali Mussa akit oa maelekezo kwa Maofisa, Wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Morogoro mjini tarehe 07.04.2020 alipokua katika ziara ya kukagua uwepo wa askari Kata na kukagua utekelezaji wa dhana ya Ushirikishwaji wa Jamii.
Kamishina wa Ushirikishwaji wa Jamii, Dkt Mussa Ali Mussa akit oa maelekezo kwa Maofisa, Wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Morogoro mjini tarehe 07.04.2020 alipokua katika ziara ya kukagua uwepo wa askari Kata na kukagua utekelezaji wa dhana ya Ushirikishwaji wa Jamii. Kushoto ni Kamanda wa Polisi MMkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Muslim na Kulia ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Mrashan Rogat.
Kamishina wa Ushirikishwaji wa Jamii, Dkt Mussa Ali Mussa akionesha kitabu cha mwongozo wa kufichua na kuzuia uhalifu kwa Polisi kata, maafisa watendaji wa kata, mitaa na vijiji. Kitabu hicho kimeandaliwa mahsusi kiwe msaada kwa Polisi kata na watendaji wengine ikiwa ni mkakati wa Jeshi la Polisi katika kupunguza uhalifu. Dkt Mussa yupo katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa uwepo wa askari kata na utekelezwaji wa dhana ya Ushirikishwaji wa Jamii katika mikoa ya Morogoro, Tanga na Pwani. Picha Na Jeshi la Polisi