Mwenyekiti wa baraza la Vyama vya Siasa hapa nchini, John Shibuda,akisaini kitabu cha Maombolezo ya aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano Hayati Dkt.John Magufuli aliyefarika Machi 17,2021 jijini Dar es Salaam katika Hospital ya Mzena.
Mwenyekiti wa baraza la Vyama vya Siasa hapa nchini, John Shibuda,akizungumza na waandishi wa habari April 6,2021 jijini Dodoma wakati Tafakari Maalum ya Kuhitimisha kipindi cha Maombolezo ya Kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt.John Magufuli na kutoa Salam Mahsusi za Pongezi na Hongera kwa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya waandishi wa habari Dodoma wakimsikiliza Mwenyekiti wa baraza la Vyama vya Siasa hapa nchini, John Shibuda,wakati akizungumzia Tafakari Maalum ya Kuhitimisha kipindi cha Maombolezo ya Kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt.John Magufuli na kutoa Salam Mahsusi za Pongezi na Hongera kwa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan.
……………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma.
Mwenyekiti wa baraza la Vyama vya Siasa hapa nchini, John Shibuda amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kukutana na viongozi wa baraza hilo ili kuzungumza nao kuwapa muwelekeo wa Serikali yake.
Ombi hilo amelitoa April 6,2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Mhe.Shibuda,amesema kuwa ametumia fursa hii kumuomba Rais Samia kama itampendeza awaite viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania tuje kupokea Nasaha zako.
Shibuda amesema kuwa ni muhimu kukaa pamoja na kuzungumzia tasnia ya siasa na wadau wake na wapo tayari kushirikiana na serikali katika kudumisha amani, upendo na mshikamano kwa kushauriana na kukosoana.
“Tukosoane sisi kwa sisi, hii iwe ni badala ya baadhi ya wadau wa siasa kutumia marafiki wa Tanzania nje wawe ndio sikio sikivu kwa maumivu ya wavaa viatu vya siasa za Tanzania,” amesema Shibuda.
Amesema kuna umuhimu wa kukaa pamoja kutafuta ufumbuzi wa kuondoa kusigana kati ya wadau wa vyama hivyo na mamlaka za dola, ni wakati wa kuwepo kwa vikao vya baraza hilo.
“Hivi vifanyike kwa mujibu wa sheria na kanuni za vyama vya siasa Tanzania, na hii iwe nia ya serikali ya awamu ya sita katika ufufuaji uhai wa demokrasia ya vyama vingi hapa nchini,” amesema.
Amebainisha kuwa viongozi na watumishi wa serikali kupandisha viwango vya sifa ya kukweza maana ya Tanzania kuwa na mfumo wa vyama vingi na vipatikane na haki zote za Katiba ya nchi.
Aidha, Shibuda amempongeza Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa hotuba yake wakati akiapisha Makatibu wakuu na Wakuu wa Taasisi kwa kuwa ngao kinga dhidi ya umma kwa kuleta matokeo chanya.
“Matendo haya ni uamsho mpya unaokweza morali na kukuza ari mpya ya umma kuwa rafiki na serikali hii ya Rais Samia, nampa hongera sana kwa hatua zake alizoelekeza zitimizwe na utumishi wa awamu ya serikali yake,” amesema.
Kuhusu mambo yaliyofanywa na Hayati Rais John Magufuli, Shibuda amesema ataenziwa kwa mambo mengi aliyoyafanya kwa nchi yake ambapo watanzania kwasasa wanafahamu Tanzania ukombozi wake hautowajibikiwa kifikra na matendo na taasisi za nje.