*****************************
Na, Said Hauni, Lindi
April 05:UONGOZI wa Kijiji cha Mchichili,Wilaya ya Ruangwa,Mkoa wa Lindi, umetaja changamoto zinazodaiwa kukwamisha usimamizi na utunzaji wa Misitu ni wafugaji na wakulima kuvamia maeneo ya hifadhi kufanya shughuli zao za kibinaadamu.
Afisa Mtendaji wa Kijiji hich,Husna Kijazi,ameyaeleza hayo katika mahojiano maalum na timu ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari ilipotembelea Kijijini hapo kuona shughuli za kimaendeleo zinazofanywa na Jamii.
Kijazi amesema changamoto nyingi inazoikabili hifadhi ya Misitu iliyopo katika maeneo ya Kijiji hicho,ni pamoja na uvamizi wa mifugo unaofanywa na wafugaji,wakulima na uvunaji haramu wa mazao yanayotokana na Misitu na kukosekana kwa Soko la uhakika kwa Jamii ya Miji isiyofahamika.
Kijazi alisema iwapo serikali itakipa kijiji hicho kipaumbele cha kuvuna,kununua na kuuza mazao yanayotokana na Misitu iliyopo kwenye hifadhi ya vijiji kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo,kutasaidia kukuza soko la ndani na kupunguza tatizo hilo kwa jamii.
Pia,ameshauri ni vizuri kamati za Mali asili zikapewa Mafunzo ya mgambo ili kusaidia uvamizi wa uvunaji haramu wa rasilimali misitu na wafugaji kuendelea kuvamia bila kufuata taratibu zilizopo kutoka mamlaka husika.
Mtendaji huyo wa kijiji amesema licha ya uwepo wa changamoto hizo,yapo baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa mpango wa usimamizi shirikishi wa Misitu ya hifadhi za vijiji,ikiwemo ujenzi wa Ofisi Serikali za vijiji,Zahanati,Nyumba za kuishi walimu,vyumba vya madarasa, maabara,vyoo na utengenezaji wa madawati na ununuzi wa Trekta la kijiji.