MENEJA wa Kampuni ya Ujenzi ya Tanzania Building Works Limited
Mohammed Noray,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akitoa pongezi kwa Rais Samia kwa kufanya mabadiliko yenye tija katika baraza la Mawaziri.
MENEJA wa Kampuni ya Ujenzi ya Tanzania Building Works Limited
Mohammed Noray,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa pongezi kuchaguliwa kwa Rais Samia.
………………………………………………………………………….
Tuna Imani kubwa na Mama,tutachapa kazi! Ni kauli iliyotolewa na Meneja wa Kampuni ya Ujenzi ya Tanzania Building Works Limited Mohammed Noray,amesema kuwa wanaimani kubwa na wanampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania kwani ataendeleza kujenga Taifa lililo bora kwa kuleta maendeleo.
Aidha amempongeza kwa kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri kwani amechagua na Baraza lililomakini na litaendelea na kazi ya kumsaidia katika kuleta maendeleo na kusimamia vyema kwa kuwaletea maendeleo na Taifa kwa ujumla.
Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati akiongea na waandishi wa habari Bw.Noray,amesema kuwa ana imani na Rais Samia na kwamba hatawangusha watanzania kwa sababu alifanya kazi kwa karibu na mtangulizi wake hayati Rais Dkt,John Pombe Magufuli .
“Tayari tumeanza kuona vitendo,tumeona jinsi ambavyo ameanza kuchukua
hatua na kukemea mambo ambayo anaona hayafai na hayana tija kwa Taifa
na wananchi.”amesema.
Pia alitumia fursa hiyo kumponmgeza Rais Samia kwa kumteua Dkt.Philip
Mpango na baadaye kupata Baraka za wabunge na kuwa Makamu wa Rais ambaye kimsingi amesema atamsaidia sana kwani Dkt.Mpango ni mchapa kazi na mwadilifu.
“Tuendelee kumuombea Rais wetu huyu aweze kutufikisha pale
tunapopataka hasa katika kusimamia kikamilifu miradi mbali ikiwemo
miradi mikubwa aliyoiacha hayati Rais Dkt.John Magufuli na changamoto zinazowakabili
wananchi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla .
Aidha Bw.Noray,ametoa rai kwa waliopewa dhamana na Rais Samia Mawaziri kutokumuangusha na badala yake wafanye kazi kwa kufuata sheria ,taratibu na kanuni za nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Hata hivyo ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa Rais Samia na watanzania wote kwa kuondokewa aliyekuwa Rais wa Nchi hayati Dkt.John Magufuli huku akiwaasa kuendelea kuienzi kazi kubwa aliyoifanya hasa katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali na miradi mikubwa ya maendele ya nchi.
“Tumuenzi Dkt.Magufuli kwa vitendo hasa katika kuwatetea wanyonge lakini pia kutambua mchango wa watanzania ambao walikuwa wakifanya kazi kwa kushirikiana na Serikali katika miradi katika nyanja na sekta mbalimbali.”amesisitiza
Pia ametoa wito kwa wafanyabaishara waliokuwa wamefunga maduka yao na kwenda nje warudi nchini kwani Tanzania ni nchi yenye Amani na inawapenda wafanyabiashara waache kusikiliza maneno ya watu.